Uganda kuteketeza dozi 400,000 za chanjo za covid

Muhtasari

•Uganda kuteketeza dozi 400,000 za chanjo za covid

Image: GETTY IMAGES

Uganda inatarajia kuteketeza chanjo 400,000 za virusi vya corona ambazo hazijatumika, zilizokuwa zimetolewa kwa matumizi kaskazini mwa nchi hiyo.

Dozi nyingi ambazo hazijatumika ni Moderna na Astrazeneca.

Dozi hizo zinatajwa kuisha muda wake, kwa mujibu wa gazeti la mtandaoni la Uganda, Monitor.

Hatua hii inakuja wakati nchi imefikia chini ya nusu la lengo lake la kutoa chanjo kwa watu milioni 22, chanzo hicho hicho kilisema.

"Moderna imeganda sana - inapaswa kuyeyushwa. Kabla ya matumizi, wakati haikutumika huko Acholi tuliipeleka hadi Magharibi mwa Uganda lakini hatukuweza kuitumia kabla ya siku 30," tovuti ya habari nchini Uganda Nile Post inamnukuu Waziri wa Afya Jane Aceng alisema.

Alihusisha uchukuaji mdogo wa chanjo na taarifa za kusadikika za kiafya, iliendelea.