Uvamizi wa Ukraine: Urusi yaonya kuwa itashambulia maeneo maalum mjini Kyiv

Muhtasari
  • Urusi yaonya kuwa itashambulia maeneo maalum mjini Kyiv
Image: EPA

Wizara ya ulinzi ya Urusi imetoa onyo kwa wakazi wa Kyiv kwamba inajiandaa kushambulia maeneo maalum katika mji mkuu wa Ukraine.

Katika taarifa iliyotolewa leo mchana, maafisa wa Urusi walisema vikosi vyao vinajiandaa kufanya "mashambulizi ya uhakika na ya hali ya juu" dhidi ya "vituo vya kiteknolojia vya Huduma ya Usalama ya Ukraine na kituo kikuu cha 72 cha PsyOps huko Kyiv".

"Tunawahimiza raia wa Ukraine ambao wanatumiwa na watu wa kitaifa kutekeleza uchochezi dhidi ya Urusi, pamoja na wakaazi wa Kyiv wanaoishi karibu na vituo vya hivyo kuondoka nyumbani kwao," iliongeza taarifa hiyo.

Maafisa walidai mashambuli hilo linafanywa ili "kuzuia mashambulizi ya mawasiliano dhidi ya Urusi".

Huku hayo yakijiri Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Oleksiy Reznikov ameonya kuhusu uwezekano wa Urusi kufanya "shambulio la kisaikolojia".

Bw. Reznikov alidai kwenye mtandao wake wa Facebook kuwa Urusi ikwanza inapanga kuvuruga mawasiliano.

"Baada ya hapo, kutakuwa na usambazaji mkubwa wa taarifa ghushi kuhusu uongozi wa kijeshi na kisiasa wa Ukraine," aliandika.