Ukraine kupokea vifaru vya Czech na makombora ya $100m ya Javelin kutoka Marekani

Muhtasari

• Jamhuri ya Czech imeripotiwa kuwa nchi ya kwanza ya Umoja wa Ulaya kuipatia Ukraine moja kwa moja silaha za kivita tangu uvamizi wa Urusi uanze siku 41 zilizopita.

• Marekani yaahidi $100m nyingine katika makombora ya Javelin.

 

Image: Getty Images

Jamhuri ya Czech imeripotiwa kuwa nchi ya kwanza ya Umoja wa Ulaya kuipatia Ukraine moja kwa moja silaha za kivita tangu uvamizi wa Urusi uanze siku 41 zilizopita.

Maafisa wakuu wa Czech waliliambia shirika la habari la Reuters kwamba nchi hiyo imetuma vifaru vya T-72 vilivyotengenezwa na Soviet na magari ya kivita ya BVP-1 kwenda Ukraine, na kuthibitisha ripoti za vyombo vya habari vya ndani ambazo zilionyesha treni iliyosheheni vifaru vitano na magari matano ya mapigano.

Waziri wa Ulinzi Jana Cernochova aliliambia bunge kuwa hatathibitisha au kukataa maelezo ya msaada wa Czech kwa Ukraine.

"Nitawahakikishia tu kwamba Jamhuri ya Czech...inasaidia Ukraine kadri inavyoweza na itaendelea kusaidia kwa (kusambaza) zana za kijeshi, nyepesi na nzito," Jana Cernochova alisema.

Inakuja huku kukiwa na ripoti kwamba serikali ya Ujerumani mapema wiki hii iliondoa pingamizi dhidi ya mfanyabiashara binafsi wa silaha wa Czech anayesafirisha magari56 ya kijeshiyaliyoundwaUjerumani Mashariki hadi Ukraine.

Marekani yaahidi $100m nyingine katika makombora ya Javelin

Katika duru ya hivi punde ya usaidizi wa kijeshi wa Marekani kwa Ukraine, maafisa wa Marekani walisema Jumanne kwamba watatoa $100m (£76m) za makombora javelin ya kukinga silaha kwa vikosi vya Ukraine.

Hili ni kundi la sita la msaada wa vifaa vya Marekani kutolewa kwa Ukraine tangu Agosti.

Ahadi ya hivi punde ina maana kwamba $1.7bn ya vifaa vya kijeshi imeahidiwa kwa Ukraine na Marekani pekee tangu mashambulizi ya Urusi kuanza tarehe 24 Februari, kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.

Msemaji wa Pentagon ya Marekani John Kirby alisema katika taarifa yake kwamba fedha hizo mpya zilizoidhinishwa "zitakidhi hitaji la dharura la Ukraine la kuongeza mifumo ya kuzuia silaha za Javelin , ambayo Marekani imekuwa ikitoa kwa Ukraine na wamekuwa wakitumia kwa ufanisi kuilinda nchi yao. ".