Mariupol:'Kizibeni hata nzi asitoke', Putin aamuru

Muhtasari

• Putin alisema "hakuna haja ya kupanda kwenye makaburi haya na kutambaa chini ya ardhi kupitia vituo hivi vya viwanda".

• Badala yake, ametoa wito kwa vikosi vyake "kuziba eneo hili la viwanda ili hata inzi asitoroke".

Rais Putin na waziri wake wa ulinzi
Rais Putin na waziri wake wa ulinzi
Image: Russian Pool

Kufuatia hatua ya Rais wa Urusi Vladimir Putin kufuta mipango ya kuvamia kiwanda cha chuma cha Azovstal huko Mariupol, ambapo wanajeshi wa mwisho wa Ukraine katika mji huo wamekuwa wakishikilia dhidi ya uvamizi wa Urusi.

Katika mkutano wa televisheni, kwenye meza ndogo kutoka kwa waziri wake wa ulinzi, Putin alisema "hakuna haja ya kupanda kwenye makaburi haya na kutambaa chini ya ardhi kupitia vituo hivi vya viwanda".

Badala yake, ametoa wito kwa vikosi vyake "kuziba eneo hili la viwanda ili hata inzi asitoroke".

Aliongezea haiteleweka kuvamia eneo kubwa lenye viwanda , ambapo zaidi ya wanajeshi 2000 wa Ukraine wanaripotiwa kuwepo na kwamba uamuzi huo ulikuwa unafanywa kulinda usalama wa wanajeshi wa Urusi.

Putin aliwasifu wanajeshi wa Urusi kwa ‘kuuweka huru’ mji wa Mariupolbaada ya waziri wa ulinzi Sergei Shoigu kumwambia kwamba wanajeshi wa taifa hilo wanadhibiti mji huo wa bandari wa Ukraine ijapokuwa bado kuna makabiliano kukiteka kiwanda hicho.