Tanzia! Mwanahabari sifika wa Al Jazeera auawa kwa kupigwa risasi usoni

Muhtasari

• Shirleen ambaye alikuwa na umri wa miaka 51 aliuawa katika eneo la West Bank alipokuwa akiripoti kuhusu oparesheni ya wanajeshi wa Isarel katika kambi ya wakimbizi ya Jenin.

• Kituo cha habari cha Aljazeera katika taarifa yake kilisema kwamba Abu Akleh fariki katika “mauaji ya kinyama” na kutaka jamii ya kimataifa kuhakikisha kuwa jeshi la Israel linawajibikia mauaji hayo.

• Israel pia ilipendekeza kufanyika kwa uchunguzi wa pamoja baina yao na Palestina ili kubaini mauaji ya mwanahabari huyo.

Shireen Abu Akleh, mwanahabari mkongwe wa Kipalestina wa Al Jazeera, alipigwa risasi usoni wakati wa uvamizi katika kambi ya wakimbizi ya Jenin [Al Jazeera]
Shireen Abu Akleh, mwanahabari mkongwe wa Kipalestina wa Al Jazeera, alipigwa risasi usoni wakati wa uvamizi katika kambi ya wakimbizi ya Jenin [Al Jazeera]

Mwanahabari mzoefu wa Al Jazeera Shireen Abu Akleh ameuawa na watu wanaoaminka kuwa wanajeshi wa Israel kulingana kituo cha habari cha Al Ajazeera.

Shirleen ambaye alikuwa na umri wa miaka 51 aliuawa katika eneo la West Bank alipokuwa akiripoti kuhusu oparesheni ya wanajeshi wa Isarel katika kambi ya wakimbizi ya Jenin.

Alifariki papo hapo baada ya kupigwa risasi moja usoni licha ya kwamba alikuwa amevalia jezi yenye nembo ‘PRESS’.

Mwanahabari mwingine raia wa Palestina, Ali al-Samoudi alijeruhiwa mgongoni lakini hali yake ni thabiti.

Kituo cha habari cha Aljazeera katika taarifa yake kilisema kwamba Abu Akleh fariki katika “mauaji ya kinyama” na kutaka jamii ya kimataifa kuhakikisha kuwa jeshi la Israel linawajibikia mauaji hayo.

Wakati huo huo Israel ilikanusha madai hayo na kudai kwamba mwanahabari huyo aliuawa na wapiganaji wa Palestina.

Israel pia ilipendekeza kufanyika kwa uchunguzi wa pamoja baina yao na Palestina ili kubaini mauaji ya mwanahabari huyo.

Palestina hata hivyo ilikatalia mbali pendekezo hilo la Israel.

Marehemu Abu Akleh ni mwanahabari mwenye tajiriba ya juu na amekuwa na ufahamu wa hali juu kuhusu mzozo wa Palestina na Israel ambapo ameripoti kuhusu mzozo huo kwa miaka mingi.