Ukraine na Urusi: Mamia ya wanajeshi wa Ukraine waliozingirwa Mauripol waliokolewa

Muhtasari

• Wapiganaji walioondolewa kutoka Mariupol wakiwasili katika mji unaodhibitiwa na Urusi.

• Naibu waziri wa ulinzi Hanna Maliar alisema kuwa wanajeshi walioumia vibaya 53 walipelekwa katika mji wa Novoazovsk.

• Awali Urusi ilisema mkataba umefikiwa wa kuwakomboa wanajeshi waliojeruhiwa.

Picha zimekuwa zikijitokeza zinazoonyesha wanajeshi wa Ukraine waliojeruhiwa hwakiwasili katika mji unaodhibitiwa na waasi wanaoungwa mkono na Urusi wa Novoazovsk,
Picha zimekuwa zikijitokeza zinazoonyesha wanajeshi wa Ukraine waliojeruhiwa hwakiwasili katika mji unaodhibitiwa na waasi wanaoungwa mkono na Urusi wa Novoazovsk,
Image: Reuters

Wapiganaji walioondolewa kutoka Mariupol wakiwasili katika mji unaodhibitiwa na Urusi.

Ukraine imethibitisha kwamba mamia ya wapiganaji wake waliokuwa wamekwama kwa zaidi ya miezi miwili katika mji wa shughuli za viwanda vya chuma wa Azocstal katika Mauripol wameokolewa.

Naibu waziri wa ulinzi Hanna Maliar alisema kuwa wanajeshi walioumia vibaya 53 walipelekwa katika mji wa Novoazovsk, unaoshikiliwa na wasi wanaoungwa mkono na Urusi.

Aisema kuwa wengine 211 walikombolewa kwa kutumia njia za kibinadamu kuelekea Olenivka – mji mwingine unaodhibitiwa na waasi.

Awali Urusi ilisema mkataba umefikiwa wa kuwakomboa wanajeshi waliojeruhiwa.

Takriban basi kumi na mbili zilizowabeba wapiganaji wa Ukraine waliokuwa wamekwama katika kiwanda kilichozingirwa zilionekana zikiondoka kusini mwa mji huo wa bandari Jumatatu jioni, liliripoti shirika la habari la Reuters.