Njaa inasababisha kifo ’kila sekunde 48’ Katika Afrika Mashariki

Muhtasari

• Ripoti ya mashirika ya misaada Oxfam na Save the Children inakadiria kuwa takriban watu milioni 181 kote duniani wanapitia uzoefu viwango vya mzozo wa njaa.

 

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yameonya juu ya njaa kali inayosababisha utapiamlo inayohusiana na mzozo, mzozo wa hali ya hewa, na mfumuko wa bei za chakula.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yameonya juu ya njaa kali inayosababisha utapiamlo inayohusiana na mzozo, mzozo wa hali ya hewa, na mfumuko wa bei za chakula.
Image: Getty Images

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yameonya katika eneo lote la mataifa ya Ethiopia, Kenya na Somalia, mtu mmoja hufariki kila sekunde 48 kutokana na njaa ya muda mrefu inayosababishwa na mzozo, mzozo wa hali ya hewa na kuongezeka kwa gharama ya chakula.

Ripoti ya mashirika ya misaada Oxfam na Save the Children inakadiria kuwa takriban watu milioni 181 kote duniani wanapitia uzoefu viwango vya mzozo wa njaa, huku wanawake wakiathiriwa zaidi.

Mashirika hayo yanasema njaa kali ni kushindwa kisiasa.

Yanakosoa jamii ya kimataifa kwa kuchelewa sana kushugulikia tatizo la njaa na kutozuia dharura "zinazojirudia na kutabirika " .