Ukraine yatoa wito wa ulinzi wa anga na msaada wa silaha

Muhtasari

•Ukraine wanasema wanahitaji sana mifumo zaidi ya silaha, huku mapigano katika eneo la mashariki la Donbas yakiendelea.

Image: BBC

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametoa wito wa kuwekewa kwa mifumo ya kisasa ya ulinzi wa makombora kwa nchi yake akisema kuwa zaidi ya makombora 2,600 yametua nchini mwake tangu kuanza kwa uvamizi huo.

Mifumo ya Iron Dome wa Israeli na American Patriot batteries ndio aina ya mifumo ambayo Zelensky anasema nchi yake inahitaji.

Makombora ya umbali mrefu ya Urusi yamekuwa wakirushwa kuelekea Ukraine tangu kuanza kwa vita hivi, wakati mengi yamedunguliwa, mengi zaidi yamefanikiwa kutua nchini humo.

Lakini ulinzi wa anga sio jambo pekee ambalo Waukraine wanataka.

Wanasema wanahitaji sana mifumo zaidi ya silaha, huku mapigano katika eneo la mashariki la Donbas yakiendelea.

Mapigano ya Severodonetsk yamegeuka kuwa vita vya umwagaji damu mitaani, na hasara kubwa zimeripotiwa pande zote mbili.

Miongoni mwao ni mwanajeshi wa zamani wa Uingereza, aliyeuawa Ijumaa iliyopita.

Mshauri wa Rais Zelensky alitoa pongezi kwa Jordan Gatley, akisema “alikuwa shujaa wa kweli.” Mykhailo Podolyak alisema: “Siku zote tutakumbuka mchango wake katika ulinzi wa Ukraine na ulimwengu huru.”