Waandishi habari wakuu wa Uingereza wapigwa marufuku Urusi

Muhtasari

•Mwandishi wa BBC Clive Myrie, Orla Guerin, Nick Robinson na Nick Beake, ambao wameripoti kutoka Ukraine, na Mkurugenzi Mkuu Tim Davie wako kwenye orodha hiyo.

•Urusi imechukua hatua hii kujibu hatua za Uingereza za kuwawekea vikwazo maafisa wakuu wa Urusi.

Waandishi wa habari wa BBC Nick Beake, Orla Guerin na Clive Myrie wote wameripoti kuhusu vita hivyo wakiwa Ukraine
Waandishi wa habari wa BBC Nick Beake, Orla Guerin na Clive Myrie wote wameripoti kuhusu vita hivyo wakiwa Ukraine
Image: BBC

Urusi imewapiga marufuku waandishi wakuu wa habari kutoka Uingereza mbali na maafisa wa ulinzi kuingia nchini humo kama sehemu ya vikwazo vyake, kujibu hatua za Uingereza za kuwawekea vikwazo maafisa wakuu wa Urusi.

Mwandishi wa BBC Clive Myrie, Orla Guerin, Nick Robinson na Nick Beake, ambao wameripoti kutoka Ukraine, na Mkurugenzi Mkuu Tim Davie wako kwenye orodha hiyo.BBC "itaendelea kuripoti kwa uhuru na haki", msemaji alisema.

Sky TV, Times, Guardian, Channel 4 na waandishi wa habari wa ITV pia wamepigwa marufuku.

Urusi tayari imewapiga marufuku mamia ya wabunge wa Uingereza .Wizara ya mambo ya nje huko Moscow ilitangaza kwamba mpango wa kupanua orodha hiyo, ambayo inajumuisha wanachama 29 wa vyombo vya habari na watu 20 "wanaohusishwa na ulinzi wa taifa hilo ", itaendelea.

"Waandishi wa habari wa Uingereza waliojumuishwa kwenye orodha wanahusika katika usambazaji wa makusudi wa habari za uwongo na za kupotosha kuhusu Urusi na matukio ya Ukraine na Donbas," wizara ya mambo ya nje ya Urusi ilisema.

"Kwa tathmini zao za upendeleo pia wanachangia kuchochea phobia ya Kirusi katika jamii ya Uingereza."