Mwanaume afungwa jela kwa kumuoa mke wa pili

Muhtasari

•Watetezi wa haki za wanawake wanasema uamuzi huo wa mahakama utawazuwia wanawake kuoa wake zaidi ya mmoja.

•Nchini Pakistan wanaume wanaweza kuoa wake wengine, lakini kwanza ni lazima waombe idhini kwa mke wa kwanza.

Image: GETTY IMAGES

Mahakama ya Pakistan imemuhukumu mwanaume kifungo cha miezi sita kwa kuoa mke wa pili bila ruhusa ya mke wa kwanza.

Mke wa mwanaume huyo kwa jina Saqib, Bi Ayesha Bibi, alishinda kesi hiyo, alipodai kuwa kitendo cha mume wake kuoa mke wa pili bila yeye kumpatia ruhusa ya maandishi , kilikuwa ni ukiukaji wa sheria ya familia nchini Pakistan.

Jaji alimuamuru mwanaume huyo kulipa faini ya dola 2,000.

Watetezi wa haki za wanawake wanasema uamuzi huo wa mahakama utawazuwia wanawake kuoa wake zaidi ya mmoja. Pia wanasema kuwa utawajengea uwezo na kuwawezesha wanawake kwernda mahakamani kudai haki yao.

"Inatia moyo kwamba mwanamke aliyenyanyaswa amelipeleka hili mahakamani," alisema Romana Bashir, kuu wa mradi wa amani na maendelea nchini humo. "Uamuazi huu unawapa uwezo wanawake," aliongeza.

 kabla ya kuoa mke mwingine.