(Video) Kiongozi wa junta wa Burkina afanya mazungumzo na rais aliyepinduliwa

Muhtasari

• Mkuu wa kundi la kijeshi linalotawala Burkina Faso amekutana na rais aliyempindua mwaka huu, kwa mazungumzo ya kujaribu "kutuliza" hali ya kisiasa.

Mkuu wa kundi la kijeshi linalotawala Burkina Faso amekutana na rais aliyempindua mwaka huu, kwa mazungumzo ya kujaribu "kutuliza" hali ya kisiasa. 

Roch Marc Christian Kabore, rais aliyechaguliwa hadi kupinduliwa kwake Januari, aliandamana na rais mwingine wa zamani Jean-Baptiste Ouedraogo (Novemba 1982 - Agosti 1983) wakati wa mkutano katika ikulu ya rais. 

Bw KaborĂ© alisalimiana na luteni kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba na kuzungumza naye katika hali ya utulivu. Ofisi ya rais ilisema katika taarifa kwamba watatu hao walijadili "masuala ya usalama, usimamizi wa mpito na masuala mengine ya maslahi ya taifa".  Ni "mwanzo wa msururu wa hatua kwa nia ya kutuliza hali ya kisiasa", iliongeza. 

Kuungana dhidi ya ugaidi 

Mkutano huo ulionyesha "hamu ya upatanisho" ya kiongozi mpya na "Burkina iliyoungana, iliyoazimia na inayounga mkono vita dhidi ya kundi la kigaidi.  

Kama Mali na nchi jirani ya Niger, Burkina inakabiliwa na msururu wa ghasia zinazolaumiwa zaidi na wanajihadi wanaohusishwa na kundi la Islamic State au Al-Qaeda. 

Utawala mpya unaoongozwa na kiongozi wa kijeshi Luteni Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba umeapa kurejesha usalama, ukimlaumu Kabore kwa kutofanya vya kutosha kuyaondoa makundi ya wanajihadi wenye silaha. 

Inasema inahitaji miaka mitatu kujenga upya nchi katika kukabiliana na waasi wa jihadi kabla ya kuandaa uchaguzi wa kidemokrasia. 

Vurugu zinazoendelea 

Hata hivyo, umwagaji damu umeendelea nchini humo. 

Mapema mwezi huu, zaidi ya raia 80 waliuawa katika wilaya ya kaskazini ya Seytenga katika shambulio la pili kwa mauti kuwahi kutokea nchini humo. Kabore alihamishwa kutoka kifungo cha nyumbani hadi nyumbani kwake katika mji mkuu wa Ouagadougou mapema Aprili kufuatia mapinduzi ya Januari. 

Hii ni mara yake ya kwanza kuonekana hadharani tangu Aprili, wakati kuachiliwa kwake kulipodaiwa mara kwa mara na wafuasi wake, Jumuiya ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS), Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.