Sherehe ya kuzikwa kwa jino la Lumumba yaanza DR Congo

Jino lililovikwa taji la dhahabu ndio masalia pekee ya shujaa wa uhuru wa Congo Patrice Lumumba.

Muhtasari

• Jino lake katika jeneza lililofunikwa bendera ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

• Lilirejeshwa kwa familia ya Bw. Lumumba wiki jana katika hafla iliyofanyika Brussels.

Jeneza limezunguka maeneo kadhaa ya nchi
Jeneza limezunguka maeneo kadhaa ya nchi
Image: AFP

Sherehe rasmi ya maziko inafanyika siku ya Alhamisi kwa jino la kiongozi wa uhuru wa Congo Patrice Lumumba katika mji mkuu Kinshasa.

Mabaki hayo ya jino ni ya waziri mkuu wa kwanza wa nchi hiyo ya Kiafrika, ambaye aliuawa mwaka 1961 na waasi wanaotaka kujitenga kwa kushirikiana na mamluki wa Ubelgiji.

Mwili wake uliyeyushwa kwa asidi lakini afisa wa polisi wa Ubelgiji alilihifadhi jino hilo kama kombecla dunia.

Lilirejeshwa kwa familia ya Bw. Lumumba wiki jana katika hafla iliyofanyika Brussels.

Jino hilo, katika jeneza lililofunikwa bendera ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, tangu wakati huo limezunguka maeneo kadhaa ya nchi hiyo kuruhusu watu kutoa heshima zao.

 

Maandalizi ya kumpumzisha Lumumba DRC
Maandalizi ya kumpumzisha Lumumba DRC
Image: BBC

                 Ni kwa nini ubelgiji ilitunza jino la dhahabu la shujaa wa Afrika 

Jino lililovikwa taji la dhahabu ndio masalia pekee ya shujaa wa uhuru wa Congo  Patrice Lumumba.

 Alipigwa risasi na kikosi cha kufyatua risasi mwaka 1961 kikiungwa mkono kimya kimya na utawala wa ukoloni wa Kibelgiji, mwili wake ulizikwa katika kaburi fupi, lilichimbwa na kusafirishwa  kilomita 200 (maili 125 ), akazikwa tena, akafufuliwa na halafu akakatwa vipande  vipande na hatimaye kuyeyushwa kwa asidi.  

 Kamishna wa polisi wa Ubelgiji, Gerard Soete, ambaye alisimamia na kushiriki katika kuangamiza mabaki alichukua jino, alikiri baadaye.

 Pia alizungumzia kuhusu jino la pili na vidole viwili vya maiti, lakini hivi havikupatiana. 

 Imepangwa sasa kwamba jino lake litarejeshwa kwa familia yake katika sherehe itakayofanyika katika mji mkuu wa Ubelgiji Brussels.

 Soete ambaye alitunza vipande vya  mwili ilielezea pia kuhusu tabia ya maafisa wa kikoloni wa Ulaya ya kurejesha masalia ya mwili nyumbani baada ya miongono kama kipindi cha kukumbuka kuwa kila mtu lazima atakufa.

 Lakini pia hatua hiyo ni udhalilishaji wa mwisho wa mwanaume ambaye Ubelgiji ulimchukuliwa kama adui.

 Soete, ambaye alionekana katika  makala mwaka 1999, alilielezea jino na vidole alivyovichukua kama "aina ya nyara ya uwindaji". Lugha inayoonyesha kwamba kwa polisi huyo Mbelgiji, Lumumba- ambaye alikuwa anaheshimiwa kote barani Afrika kama sauti inayoongoza ya ukombozi wa Waafrika – alikuwa binadamu wa kudharauliwa.

 Kwa binti yake Lumumba, Juliana, swali analojiuliza ni iwapo waliomuua walikuwa binamu au la. "Unahitaji kiwango gani cha chuki kufanya unyama kiasi hicho?" anauliza.

"Hii inatukumbusha kile kilichotokea kwa Wanazi, kuchukua vipande vya miili ya watu - na uhalifu dhidi ya binadamu," aliiambia BBC.

Binti yake Gerard Soete alionyesha jino, katika boksi lililofungwa kwa kufuli, kwa mpigapicha katika mwaka 2016
Binti yake Gerard Soete alionyesha jino, katika boksi lililofungwa kwa kufuli, kwa mpigapicha katika mwaka 2016
Image: JELLE VERMEERSCH

Lumumba alikuwa amepanda cheo  na kuwa Waziri mkuu akiwa na umri wa miaka 34. Alichaguliwa katika siku za mwisho za utawala wa kikoloni, aliongoza baraza la mawaziri la taifa jipya huru.

 Juni 1960, wakati wa kukabidhiana mamlaka,  Mfalme wa Ubelgiji Baudouin aliusifu utawala wa ukoloni na alizungumzia kuhusu babu yake, Léopold II, kama "mstaarabu" wa nchi.

 Hakusema lolote kuhusu mamilioni waliokufa au ambao waliofanyiwa ukatili chini ya utawala wake wakati huo wa kilichoitwa taifa huru la Congo Congo,  kama mali yake ya kibinafsi.   

 Kushindwa huku kukiri yaliyopita kulitawa miaka ya Ubelgiji kushindwa kukubali yaliyotokea, ambapo sasa ndio imeanza kukubali baada ya  kuelewa kwamba  Lumumba hakuwa msiri sana.

 Katika hotuba ambayo haikupangwa katika mpango rasmi, Waziri mkuu alizungumzia kuhusujinsi Wacongo wanavyoumizwa na  ghasia na kudhalilishwa.

 Katika hotuba hiyo iliyotolewa kwa misemo ya kusikitisha, iliyokatishwa na makofi na hadhira iliyosimama kumshukuru alipoikamilisha  alipoelezea "utumwa wa udhalilishaji ambao tumewekewa kwa nguvu".

 Wabelgiji walipigwa na butwaa, kulingana na msomi Ludo De Witte, ambaye aliandika makala ulioelezea ushahidi wa mauaji yake.

 Sijawahi kumsikia kabla  Mwafrika mweusi akidiriki  kuongea kama hivi mbele ya Wazungu. Waziri mkuu ambaye  De Witte  anasema alikuwa ameelezewa kama mwizi ambaye hakusoma katika vyombo vya habari vya ubelgiji, alionekana kama alikuwa akimuaibisha mfalme na maafisa wengine wa Ubelgiji.