(Video) Mzozo wa Ukraine: Kamera ya CCTV yaonesha watu wakitoroka kufuatia shambulio la Urusi Kremenchuk

Watu wanaonekana wakikimbia na watoto huku makombora wakirushwa kiholela

Muhtasari

• Picha za CCTV kutoka kwenye kidimbwi cha maji katika mji wa Kremenchuk nchini Ukraine zimenasa raia waliokuwa wakikimbia kujificha na kuanguka chini huku makombora ya Urusi yakishambulia.

Picha za CCTV kutoka kwenye kidimbwi cha maji katika mji wa Kremenchuk nchini Ukraine zimenasa raia waliokuwa wakikimbia kujificha na kuanguka chini huku makombora ya Urusi yakishambulia eneo jirani na kusababisha vifo vya takriban watu 18.

BBC imechambua kanda hiyo - na inaonekana kombora moja lilipiga karibu na kituo cha biashara, huku lingine likipiga kaskazini wa kiwanda cha karibu.

Urusi inadai kushambulia kituo cha kuhifadhi silaha kilichosababisha moto na kuteketeza jengo la karibu la maduka.

Maafisa wa Ukraine wamekanusha kuwa kulikuwa na ghala la silaha karibu.