(Video) Vita vya Ukraine: Mwanamke Mrusi aokolewa kutoka eneo la bomu, Kyiv

Muhtasari

• Familia ya Urusi na Ukraine imegawanyika kutokana na vita nchini Ukraine baada ya raia wa Urusi Ekaterina Volkova kujeruhiwa katika shambulio la anga.

Familia ya Urusi na Ukraine imegawanyika kutokana na vita nchini Ukraine baada ya raia wa Urusi Ekaterina Volkova kujeruhiwa katika shambulio la anga na mumewe kuuawa katika shambulio hilo hilo. 

Hii ilikuwa mara ya pili kwa Urusi kudondosha kombora kwenye jengo lao la ghorofa. Mwishoni mwa Aprili, mwandishi wa habari wa Radio Liberty aliuawa katika jengo hilo hilo. 

Mamlaka ya Ukraine ilisema tukio hilo lilionyesha shambulio la bomu la Urusi lilikuwa likilenga hata raia wao. 

Mwandishi wa BBC Anastassiya Zlatopolskai ameifuatilia familia hiyo mjini Kyiv ambayo inasema shambulio hilo haliwezi kusamehewa.

IMETAFSIRIWA NA DAVIS OJIAMBO.