Mauji ya Shinzo Abe: Mwili wa Waziri mkuu wa zamani wa Japan warejeshwa nyumbani

Abe alipigwa risasi na kuuawa alipokuwa akizungumza katika mkutano wa kampeni ya kisiasa Ijuamaa kusini mwa mji wa Nara.

Muhtasari
  • Polisi wanaochukuza mauaji yake wanasema mshukiwa aliyefyatua risasi aliwaambia maafisa kwamba alikuwa na chuki dhidi ya ‘’shirika maalum’’

Gari lililoubeba mwili wa Waziri mkuu wa zamani wa Japan Shinzo Abe limewasili nyumbani kwake katika mji mkuu wa Tokyo.

Abe alipigwa risasi na kuuawa alipokuwa akizungumza katika mkutano wa kampeni ya kisiasa Ijuamaa kusini mwa mji wa Nara.

Polisi wanaochukuza mauaji yake wanasema mshukiwa aliyefyatua risasi aliwaambia maafisa kwamba alikuwa na chuki dhidi ya ‘’shirika maalum’’

Yamagami aliamini Shinzo Abe alikuwa sehemu ya kundi hilo, ndiyo maana alimpiga risasi, wanaongeza.

Alipoulizwa na mjumbe wa vyombo vya habari vya Japan kama nia ya mpiga risasi huyo ilikuwa kumuua Abe, polisi wanasema tu kwamba Yamagami alikiri kumpiga risasi Waziri Mkuu huyo wa zamani.

Waziri mkuu wa sasa Fumio Kishida anatarajiwa kutembele eneo la tukio leo mchana.

Kulingana na taarifa za vyombo vya habari nchini humo, kutakuwa na mkesha siku ya Jumatatu na mazishi ya Bw Abe yatafanyika Jumanne.

Abe walikuwa Waziri mkuu aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi nchini Japan na kifo chake ambacho kimetokea akiwa na umri wa miaka 67, kimewashtua wengi katika nchi hiyo ambako visa vya uhalifu wa bunduki ni nadra sana.

Aliawa alipokuwa akifanya kampeni kwa ajili ya chama chake katika uchaguzi wa bunge wa Jumapili.