Aliyekuwa mke wa Donald Trump, Ivan Trump amefariki

Alikuwa pia Mwanariadha wa kiwango cha Kimataifa

Muhtasari

•Donald, ambaye  alikuwa bwana wa  Ivana kutoka 1977 hadi 1992, pia hakuficha hisia zake kumwomboleza bibi yake huyo wa zamani. 

•Mwili wa mwendazake ilipelekwa kwa  hospitalini  kwa Mkuguzi wa Afya ili kubaini chanzo  cha kifo chake.

Ivana Trump mke wa Rais wa Zamani wa Merekani Donald Trump
Ivana Trump mke wa Rais wa Zamani wa Merekani Donald Trump
Image: ICON IMAGES

Ivana Trump, mke wa zamani wa Rais wa zamani Donald Trump, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 73, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa watoto wake Donald Trump Jr., Ivanka Trump na Eric Trump.

''Ni kwa masikitiko makubwa  kutangaza kifo cha mama yetu  mpendwa," Ivan Trump alisema kwa taarifa, "Mama yetu alikuwa mwanamke  aliyemiliki biashara na kando na hayo,pia alikuwa mwanariadha wa kiwango cha kimataifa, mama alikuwa na mapenzi ya dhati kwa watu na kujali na rafiki zake,"

Mwanariadha huyo amewacha pengo kubwa kwa familia yake ya watoto wa  tatu na  wajukuu kumi.

Donald, ambaye  alikuwa bwana wa  Ivana kutoka 1977 hadi 1992, pia hakuficha hisia zake kumwomboleza bibi yake huyo wa zamani. 

"Nina huzuni kubwa kuwajulisha wote waliompenda, ambao ni wengi, kwamba Ivana Trump amefariki nyumbani kwake huko New York City," aliandika. "Alikuwa mwanamke mzuri, mrembo, na wa kushangaza, ambaye aliishi maisha mazuri,"

Aliongeza kwa kusema kuwa , "Fahari na furaha yake ilikuwa watoto wake watatu, Donald Jr., Ivanka, na Eric. Aliwajivunia sana,Mungu alaze roho wake pahali pema peponi,"

Kulingana na Afisa wa jiji la New York  walisema kuwa Ivana alipatikana amekufa ndani ya nyumba yake Manhattan mnamo Julai 14.

Mwili wa mwendazake ilipelekwa kwa  hospitalini  kwa Mkuguzi wa Afya ili kubaini chanzo  cha kifo chake.