Mkuu wa zamani wa Al-Shabab ateuliwa katika nafasi ya juu ya uwaziri

Robow pia aliwahi kuwa msemaji wa Al-Shabab.

Muhtasari

•Amekuwa chini ya kizuizi cha nyumbani baada ya maafisa wa rais wa zamani kumkamata kutoka Baidoa ambako alikuwa akijaribu kusimama ugavana.

•Mukhtar Robow aliondoka kwenye kundi hilo mwaka 2015 akitaja tofauti za kiitikadi na kuunda kundi lake ambalo lilikuwa likipigana dhidi ya Al-Shabab.

Image: BBC

Aliyekuwa namba mbili katika tabaka la utawala kwenye kundi la Al-Shabab, Mukhtar Robow, ameteuliwa katika nafasi ya juu ya uwaziri nchini Somalia.

Robow pia aliwahi kuwa msemaji wa Al-Shabab.

Amekuwa chini ya kizuizi cha nyumbani baada ya maafisa wa rais wa zamani kumkamata kutoka Baidoa ambako alikuwa akijaribu kusimamia ugavana wa eneo hilo mnamo Desemba 2018.

Mukhtar Robow - anayejulikana pia kama Abu Mansoor - alijisalimisha kwa serikali ya Somalia mnamo Agosti 2018 na ndiye mwanachama wa ngazi ya juu zaidi wa Al Shabaab kuhama kundi hilo.

Alikamatwa mnamo Desemba 2018 alipokuwa akifanya kampeni za kuwania kiti cha juu cha ukanda wa Kusini Magharibi.

Kufuatia kukamatwa kwake, taarifa ya serikali ilisema amekuwa akiandaa wanamgambo huko Baidoa.

Na alishutumiwa kwa kutoacha itikadi zake za itikadi kali.

Zaidi ya watu 20 waliuawa ghasia zilipozuka baada ya kukamatwa kwake.

Mukhtar Robow aliondoka kwenye kundi hilo mwaka 2015 akitaja tofauti za kiitikadi na kuunda kundi lake ambalo lilikuwa likipigana dhidi ya Al-Shabab.

Mnamo mwezi Juni, 2017 Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilimwondoa mwanamgambo huyo aliyefunzwa na Al Qaeda kwenye orodha yake ya magaidi na kubatilisha zawadi ya dola milioni tano kwa atakayewezesha kukamatwa kwake.

Sasa yeye ni Waziri wa Masuala ya Kidini ambayo inaweza kumaanisha tangazo la vita vya kiitikadi dhidi ya AL-Shabab lakini wengine wanaona ni kuficha uhalifu uliofanywa chini ya uangalizi wake wakati akiwa kiongozi wa kikundi chenye uhusiano na Al-Qaida.

Kundi hilo linafanya kazi katika maeneo mengi ya Somalia, Kenya na kwingineko katika Afrika Mashariki.

Robow ni nani?

  • Bwana Robo alikuwa naibu kiongozi wa al-Shabaab na msemaji wa kundi hilo la wapiganaji wa kiislamu.
  • Mnamo mwaka 2000 alipata mafunzo katika kundi la kijihadi la al-Qaeda nchini Afghanistan.
  • Alijitoa katika al-Shabab mnamo 2012, kutokana na alichokitaja kuwa ni tofuati za mawazo na fikra.
  • Alijisalimisha pamoja na wapiganaji wake katika mji ulio kusini magharibu wa Hudur.
  • Baadaye aliliunda kundi lake la wanamgambo waliopigana vita dhidi ya Alshabaab.

Mnamo Juni mwaka jana, kufuatia taarifa kwamba Robow anashirikiana na serikali ya Somalia, Wizara ya mambo ya nje ilimuondoa katika orodha ya magaidi.