Uingereza yatayarisha mabilioni ya Pauni kusaidia silaha na kuijenga upya Ukraine

Uingereza imetenga pauni nyingine bilioni 3 kwa kusaidia usambazaji wa silaha kwa Ukraine na ujenzi mpya

Image: BBC

Mamlaka ya Uingereza imechukua hatua muhimu katika kutenga pauni nyingine bilioni 3 kwa kusaidia usambazaji wa silaha kwa Ukraine na ujenzi mpya wa nchi hiyo baada ya vita.

Televisheni ya Uingereza Sky News iliripoti kwamba Mkuu wa hazina wa Uingereza, Nadeem Zahavi, aliunga mkono utoaji wa ufadhili wa kabla ya mauzo ya nje kupitia wakala wa serikali UKEF.

"Ninaona kuwa ni muhimu sana kuendelea kusaidia mamlaka ya Ukraine kwa njia zote zinazopatikana. Ni lazima tuoneshe imani katika mustakabali wa Ukraine,” Zahavi, ambaye anasimamia sera ya bajeti ya nchi hiyo, alisema katika maoni yake kuhusu pendekezo la UKEF la kutenga fedha.

Kiasi kikubwa - £2.3bn - kitakwenda kufadhili mauzo ya nje ya ulinzi wa Uingereza kwa Ukraine, na mikopo ya £ 700m iliyobaki itaenda kwa makampuni ya Uingereza ambayo Ukraine itaalika kuijenga upya nchi baada ya uvamizi wa Urus