Uganda yapiga marufuku kundi la wapenzi wa jinsia moja

Mahusiano ya wapenzi wa jinsia moja nchini Uganda ni haramu na wanaokiuka wanaweza kufungwa maisha gerezani.

Muhtasari

•Kundi hilo la Sexual Minority Uganda { Smug} limeamriwa kufunga virago ‘’mara moja’’ kwa kutojisajili vizuri na mamlaka.

•Tangu kuanzishwa kwake karibu miongo miwili iliyopita, Smug imefanya kampeni kwa ajili ya haki za watu wa LGBT nchini Uganda .

Wapenzi wa jinsia moja Uganda
Wapenzi wa jinsia moja Uganda
Image: BBC

Maafisa wa Uganda wamelipiga marufuku kundi moja la wapenzi wa jinsia moja katika hatua inayoonekana kuwa pigo kwa jamii hiyo nchini humo.

Kundi hilo la Sexual Minority Uganda { Smug} limeamriwa kufunga virago ‘’mara moja’’ kwa kutojisajili vizuri na mamlaka.

Kundi hilo limeelezea amri hiyo kuwa unyanyasaji wa serikali dhidi ya wapenzi wa jinsia moja nchini Uganda.

Wana kampeni hao wanakabiliwa na mateso nchini humo ambapo maoni dhidi ya wapenzi wa jinsia moja ni suala la kawaida.

Mahusiano ya wapenzi wa jinsia moja nchini Uganda ni haramu , na wanaokiuka wanaweza kuadhibiwa kwa kupewa kifungo cha maisha jela , kwa kufanya makosa yasio ya kiasili

Data rasmi inaonesha kwamba takriban watu 194walishtakiwa kwa makosa hayo kati ya 2017 na 2020, ikiwemo watu 25 waliohukumiwa.

‘’Huu ni unyanyasaji wa wazi unaoshinikizwa na wale walio na imani dhidi ya wapenzi wa jinsia moja, alisema mkurugenzi wa Smug’’ , Frank Mugisha ambaye ni mwanaharakti wa wapenzi wa jinsia moja nchini Uganda.

Alishtumu mamlaka kwa kuwachukulia wanachama wa kundi hilo kama raia wa daraja la pili na kujaribu kuangamiza uwepo wao.

Siku ya Ijumaa , maafisa wa Uganda walitangazawalikuwa wanafutilia mbali operesheni za Smug kwasababu kundi hilo la kampeni lililoanzishwa 2004, lilishindwa kusajili vizuri jina lake na shirika la kitaifa la mashirika yasiokuwa ya kiserikali

Ni sababu hiyohiyo iliotolewa mwaka uliopita wakati makumi ya makundi ya wanaharakati - ikiwemo mashirika yanayopigania Demokrasia yalipigwa marufuku na serikali ya Uganda.

Wakati huu maafisa wanasema kwamba suala hilo linatokana na jina la Smug lenyewe - Sexual Minorities Uganda.

Katika taarifa, shirika la serikali linaloshughulikia mashirika yasiokuwa ya serikali lilitambua kwamba Smug lilijaribu kujisajili na mamlaka 2012 , lakini kwamba ombi hilo lilikuwa limekataliwa kwasababu jina la shirika hilo ‘halipendezi’.

Rais Yoweri Museveni ambaye amekuwa afisini tangu 1986, ametoa maoni dhidi ya wapenzi wa jinsia moja awali , ikiwemo 2016 katika mahojiano na chombo cha h abari cha CNN ambapo aliwaita wapenzi wa jinsia moja kama watu ‘wanaochukiza’.

Ijapokuwa hakuna sheria zinazoharamisha kuwa watu waliobadili jinsia nchini Uganda, watu hao mara kwa mara wanashtakiwa kwa makosa mengine ikiwa ni pamoja na kutoa uwakilishi wa kibinafsi wa uwongo, kulingana na ripoti zilizokusanywa na mashirika ya kutetea haki za binadamu.

Tangu kuanzishwa kwake karibu miongo miwili iliyopita, Smug imefanya kampeni kwa ajili ya haki za watu wa LGBT nchini Uganda kwa kukuza upatikanaji wa huduma za afya na kusaidia wanachama wa kundi hilo kuishi kwa uwazi.

Pia limechukua hatua za kisheria kuwalinda wapenzi wa jinsia moja dhidi ya uadui, ikiwa ni pamoja na mwaka 2010 lilipofanikisha ombi la hakimu wa Uganda kuamuru gazeti kuacha kuchapisha majina na picha za wapenzi wa jinsia moja nchini Uganda chini ya kichwa cha habari "wanyonge".

Kundi hilo lilisema wanachama wake kadhaa walishambuliwa au kunyanyaswa kutokana na makala hiyo - ikiwa ni pamoja na mwanamke mmoja ambaye alikaribia kuuawa na majirani zake walipoanza kurusha mawe kwenye nyumba yake.

Wakati huo, wanasiasa wa Uganda walikuwa wakijiandaa kujadili iwapo wataanzisha au kutoanzisha hukumu ya kifo kwa wapenzi wa jinsia moja - marekebisho ya sheria ambayo yalivutia shutuma nyingi za kimataifa kabla ya kuondolewa.

Hivi majuzi, Smug ilikosoa vikali hotuba dhidi ya wapenzi wa jinsia zilizotolewa na wanasiasa wa Uganda - ikiwa ni kabla ya kuelekea katika uchaguzi wa kitaifa mwaka 2021.

  1. "Wanasiasa wanatumia jumuiya ya LGBT kama kafara ili kupata uungwaji mkono na kushinda kura hali inayochochea chuki dhidi ya watu wa jinsia hiyo ," mkurugenzi wa Smug Frank Mugisha aliambia Wakfu wa Thomson Reute