Watu wawili wahukumiwa kifungo baada ya kuua simba 6 Uganda

Washtakiwa walikiri kutenda mauaji ya simba hao ili kupata fedha za kujikimu baada ya janga la Covid 19.

Muhtasari

•Wanaume wawili wamefungwa miaka 8 na miezi saba baada ya kupatikana na hatia ya kuwaua simba sita kwa kuwatilia sumu.

Image: BBC

Hakimu wa mahakama ya Buganda Road mjini Kampala Glayds Kamasanyu amewahukumu wanaume wawili miaka 8 na miezi saba baada ya kupatikana na hatia ya kuwaua simba sita kwa kuwatilia sumu.

Akitoa hukumu hiyo alisema ushahidi uliotolewa umethibitisha wawili hao waliingia mbuga ya wanyama ya Queen Erizabeth iliyoko wilaya ya Kasese magaharibi mwa Uganda mwaka jana na kuwapatia sumu simba hao.

Kwa mujibu wa hakimu Kamasanyu, mtu anayetenda makosa hayo anastahili kifungo cha maisha lakini kwa sababu washtakiwa walikiri kutenda mauaji ya simba hao 6, ili kupata fedha za kujikimu baada ya janga la Covid 19 ndiyo sababu wamepewa kifungo hicho.

Msemaji wa Mamlaka ya wanyama pori nchini Uganda Bashir Hangi ameifahamisha BBC kuwa wamefurahishwa na hukumu iliyotolewa ili kuwa fundisho kwa watu wengine wanaofanya uwindaji haramu.

Kwa pindi cha janga la covig19 mwaka 2020 hadi 2021 zaidi ya Simba 11 waliuawa na wawindaji haramu amesema Bashir Hangi.

Kukiri kwao na pia ushahidi bayana ulithibitisha kuwa wao ndio waliwaua aina ya simba wa kipekee walio na sifa ya kupanda juu ya miti hasa katika vipindi vya jua kali.

Simba hao ni adimu na wamo katika hatari ya kuangamia duniani kwani hupatikana tu tena kwa uchache katika mbuga fulani za Uganda, Tanzania, Kenya na Afrika Kusini. Ni kwa ajili hii ndipo simba hao ni kivutio kikubwa kwa watalii na hivyo kuwezesha nchi kuingiza kiasi kikubwa cha fedha za kigeni.