Gambia yaonya 'sugarmummies' wa Uingereza dhidi ya kuwapa vijana pesa kufanya mapenzi (+video)

Inasemekana kina mama wakubwa kutoka Uingereza wanatalii Gambia na kisha kununua mapenzi kutoka kwa vijana wadogo wa ufukweni.

Muhtasari

• Vijana hao wanaoranda kweney ufukwe kuwasaidia watalii nchini Gambia wanaitwa Bumsters.

• Watalii kina mama wazee kutoka Uingereza wanasemekana kuwa na mazoea ya kuenda huko ili kukata kiu yao ya mapenzi na vijaan hao.

Ukurasa wa Twitter kwa jina Africa Facts Zone wenye takribani wafuasi laki nane umeripoti kwamba taifa la Gambia limetoa tahadhari kwa wanawake wakongwe kutoka mataifa ya kigeni haswa Uingeresa dhidi ya kuenda nchini humo na kuwahadaa vijana wadogo kwa pesa kisha kutaka mapenzi nao.

Katika taarifa nyingine iliyopeperushwa na runinga ya GB News, serikali ya Gambia ilitoa onyo dhidi ya wanawake hao ajuza kutoka Uingereza wanaosafiri nchini humo kama watalii na kisha kuanza kuwarubuni vijana wa kiume wadogo ili kushiriki mapenzi nao.

Taarifa zinasema kwamba ajuza kutoka Uingereza wana mazoea ya kutalii taifa hilo lililopo kwenye ufweke wa bahari Atlantic magharibi mwa Afrika na kueneza anasa na vijana hao wadogo maskini wanaohaha kweney ufukwe angalau kutafuta riziki.

Africa Facts Zone waliripoti kwamba vijana hao wanaorubuniwa ili kutoa huduma ya ngono kwa ajuza wa Uingereza wanaitwa ‘Bumsters’ na ni hulka ambayo imekithiri nchini humo mpaka kuilazimu serikali kuingilia kati.

GB News iliripoti kwamba serikali ya Gambia iliwataka watalii kutembelea taifa hilo kwa ajili ya kujifurahisha na kujifahamisha na utamaduni wao na wala si kuenda kwa ajili ya kupoza kiu yao ya mapenzi.

Taarifa hiyo ilizua maoni kinzani kutoka kwa washikadau mbali mbali ndani na nje ya taifa la Gambia huku mtangazaji Caroline Farrow akisema kwamba pengine Gambia wanachukua hatua kama hiyo ili kusafisha sekta yao ya Utalii ambayo imekuwa ikichafuliwa kwa wakongwe hao kutafuta mapenzi katika vijana wadogo.

Farrow alisema kwamba alisoma mahali kuwa utalii wa kingono nchini Gambia unachangia 20% ya pato la taifa hilo.

Wengi wanasema kwamba ajuza hao kutafuta mapenzi kwa vijana wadogo wa Gambia ni jambo la kawaida lakini kwa uhalisia ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za ngono kwani ni kama kumrubuni mtu.