Malkia Elizabeth II: Ni lini na ni wapi mazishi yatafanyika ?

Muhtasari

• Mechi za soka katika Primia Ligi, Ligi ya soka ya England  au katika Uskochi na Ireland  Kaskazini zimeahirishwa hadi Jumanne.

Malkia Elizabeth
Malkia Elizabeth

Mwili wa Malkia utaweza kutazamwa kwa siku nne mfululizo kwa siku nne kabla ya mazishi yake Jumatatu, tarehe 19 Septemba.

 Umma utaruhusiwa kutazama jeneza katika kipindi hicho. 

Kabla ya hili kufanyika Malkia atakuwa amepumzika katika St Giles Cathedral Edinburgh, kwa saa 24 kuanzia tarehe 12 Septemba, huku watu wakiweza kutoa heshima zao za mwisho.

   Familia yake, wanasiasa na viongozi wa dunia watahudhuria mazishi yake ya kitaifa siku hiyo, ambayo itakuwa ni  siku ya mapumziko inayofahamika kama Bank holiday.

Wajumbe wa familia ya Ufalme walisimama walipokuwa njiani kutoka kwenye ibada kutazama rambi rambi za Malkia zilizoachwa nje ya Balmoral siku ya Jumamosi.
Wajumbe wa familia ya Ufalme walisimama walipokuwa njiani kutoka kwenye ibada kutazama rambi rambi za Malkia zilizoachwa nje ya Balmoral siku ya Jumamosi.
Image: REUTERS

Kutoka Balmoral, Aberdeenshire, ambako alifariki, Jeneza la Malkia liliondoka  Jumapili kuelekea  Edinburgh, likiondoka taratibu kuelekea katika Kasri la  Holyroodhouse.

Jumatano mchana, litapelekwa katika Westminster Hall. Siku nne kamili za kutazamwa na waombolezaji  zitaanza kuanzia Alhamisi, kabla ya mazishi kufanyika.

   Mazishi ya kitaifa yatafanyika saa tano  asubuhi tarehe 19, kwa maandamano yatakayofanyika katika  Windsor Castle, yakiwemo matembezi  marefu- Long Walk. Malkia atazikwa katika kanisa dogo  linalofahamika kama King George VI Memorial Chapel lililopo Windsor.

Viongozi wa nchi kutoka maeneo mbali mbali ya dunia wataalikwa kujiunga na wanafamilia ya Ufalme kukumbuka maisha na huduma ya Malkia.

Wanasiasa wa ngazi ya juu wa Uingereza wa sasa na wa zamani na mawaziri wakuu pia wanatarajiwa kuhudhuria ibada ya mazishi itakayopeperushwa kwa njia ya televisheni.

Hakuna sharti kwa waandalizi la kufuta mipango  iliyopangwa  katika siku ya mazishi lakini muongozo wa serikali unasema kuwa waandalizi wa michezo au matukio yaliyopangwa mapema wanaweza kubadili ratba zao ili kuepuka kugongana na huduma au maandamano ya kuuaga mwili.

Baadhi ya matukio yalifutwa au kuahirishwa mara baada ya kutangazwa kwa kifo cha Malkia.

Mechi za soka katika Primia Ligi, Ligi ya soka ya England  au katika Uskochi na Ireland  Kaskazini zimeahirishwa hadi Jumanne, huku michezo ya kombe la wanawake la Super Ligi, Kombe la washindi la Wanawake na kombe la dunia la wanawake la FA ikiwa imezuiwa kwa  muda, na  ratiba ya michezo ya mashindano ya farasi, gofu na masumbwi zimefutwa. 

 Migomo mikubwa iliyokuwa imepangwa kufanyika wiki ijayo ilifutwa mara moja, na muungano wa vyama vya wafanyakazi nchini Uingereza ulisema kuwa umeahirisha mkutano wake wa mwaka katika  Brighton.

 Mfalme alithibitisha  mapema Jumapili kwamba siku ya mazishi itakuwa ni siku ya mapumziko ya   bank holiday, wakati alipotangazwa rasmi kama mfalme katika Kasri la St James, London.

Katika hotuba yake, aliisifu ‘’enzi isiyo na kifani’’.

Mfalme kutembelea mataifa 

 Kabla ya mazishi Mfalme atazuru mataifa ya Uskochi, Ireland Kaskazini na Wales.

Kipindi cha maombolezo ya kitaifa  kitadumu hadi kufikia siku ya mazishi ya kitaifa, serikali imetangaza. Familia ya Ufalme itaendelea kuomboleza kwa siku saba zaidi baada ya mazishi.

Westminster Abbey ni kanisa la kihistoria ambapo wafalme wa Uingereza na Mamalkia hutawazwa – lakini hapajawahi kufanyika mazishi pale tangu karne ya 18. Mazishi ya baba yake Malkia, babu yake na bibi mzaa baba yake, Malkia Victoria, katika miaka ya 1900, yalifanyika katika Kanisa dogo la St George, Windsor.

Wakuu wa nchi kutoka maeneo yote ya dunia wataalikwa kujiunga na wanafamilia ya Ufalme kukumbuka maisha na huduma ya Malkia.

Wanasiasa wa ngazi ya juu wa Uingereza wa sasa na wa zamani na mawaziri wa kuu pia wanatarajiwa kuhudhuria ibada ya mazishi itakayopeperushwa kwa njia ya televisheni.