Polisi wa trafiki amkamata dereva wa gari la serikali kwa uendeshaji mbaya (+video)

Dereva huyo alipigwa faini ya shilingi elfu 3 pesa za Kenya kwa kosa la kuendesha gari njia mbaya ya barabara.

Muhtasari

• Wananchi walitoa maoni mbali mbali kuhusu kitendo hicho.

• "Njia hiyo imekuwa ikitumiwa vibaya na magari ya serikali kila kunapokuwa na msongamano wa magari" 

Nchini Kenya, ni kawaida kwa madereva wa magari ya serikali kuendesha bila kufuata kanuni za barabarani. Hali ni tofuait nchini Uganda.

Jarida la Daily Monitor limeripoti kwamba polisi mmoja wat rafiki nchini humo alimsimamisha dereva wa gari la serikali aliyekuwa akiendesha gari kweney upande tofauti wa barabara na kumpiga faini.

Dereva huyo ambaye ni mfanyikazi mkubwa katika serikali ya rais Museveni alipigwa faini ya shilingi laki moja pesa za Uganda, sawa na elfu 3 za benki kuu ya Kenya.

Jarida hilo kupitia ukurasa wa Twitter walitoa taarifa hizo ambazo zilipokelewa kwa furaha kubwa na watumizi wa mtandao huo. Wengi walimsifia polisi huyo kwa ukakamavu na ujasiri wake bila kubagua cheo wala nini, bali kuzingatia kazi yake kaam inavyostahili.

“Dereva wa gari la serikali UG 0663 asubuhi ya leo alinaswa na polisi wa trafiki katika Barabara ya Binaisa (kando ya mzunguko wa Mulago) na kupigwa faini ya Sh 100,000 kwa kutumia njia isiyo sahihi,” Daily Monitor waliripoti.

Wengine walisema kwamba kwa vile gari hilo ni la mtu mkubwa serikalini huenda polisi huyo akapoteza kazi yake hivi karibuni kutokana na ushawishi wa mwenye gari hilo.

“Afisa hawa waliotoa tikiti watatafuta kazi mwezi ujao,” Mmoja kwa jina Antony.

“Vizuri sana polisi wa trafiki. Njia hiyo imekuwa ikitumiwa vibaya na magari ya serikali kila kunapokuwa na msongamano wa magari. Angalau kuanzia leo haitakuwa sawa,” mwingine alimsifia.

Ahimbisibwe Collen naye aliandika, “Ndio, watu hao wanadhani kuwa wako juu ya sheria. Wanaendesha gari vibaya hata wakiwa kwenye njia mbaya, mmoja alitaka kunifahamu pale John Babiha road.”