Maambukizi ya Ebola yaongezeka Uganda huku mlipuko ukizidi ukienea

Inaaminika kuwa vifo 21 huenda vilisababishwa na virusi vya Ebola.

Muhtasari

•Huu ni mlipuko wa nne wa Ebola nchi ya Uganda kukabiliwa nao.

Image: AFP

Idadi ya watu wanaoshukiwa kuwa na Ebola inaendelea kuongezeka nchini Uganda.

Wizara ya afya inasema kumekuwa na wagonjwa 34 wanaoshukiwa kuambikizwa.

Inaaminika kuwa vifo 21 huenda vilisababishwa na virusi vya Ebola.

Timu za afya zinaendelea kufuatilia watu ambao wanaweza kuwa wamekutana nao.

Mlipuko huo ulianza katika wilaya ya kati ya Mubende lakini sasa umeenea katika wilaya mbili jirani.

Bado hakuna kesi zilizothibitishwa katika mji mkuu Kampala.

Huu ni mlipuko wa nne wa Ebola nchi ya Uganda kukabiliwa nao.

Nchi jirani zimesema ziko katika hali ya tahadhari.