Idadi ya walioambukizwa Ebola Uganda yafikia 38 - Wizara ya afya

Watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo ni 8.

Muhtasari

•Daktari Mtanzania aliyekuwa akisoma nchini Uganda ni miongoni mwa waliofariki kutokana na virusi vya Ebola.

•Daktari Mtanzania aliyekuwa akisoma nchini Uganda ni miongoni mwa waliofariki kutokana na virusi vya Ebola.

Image: BBC

Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya ebola kufikia sasa imefikia watu 38

Kulingana na ripoti mpya ya wizara ya afya nchini Uganda, aidha idadi ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo imefikia 8 baada ya watu wengine watatu kufariki.

Watu hao waliofariki wameripotiwa kutoka eneo la Mubende.

Daktari Mtanzania aliyekuwa akisoma nchini Uganda ni miongoni mwa waliofariki kutokana na virusi vya Ebola.

Raia huyo huyo mwenye umri wa miaka 37 alikuwa akisomea Shahada ya Uzamili ya Udaktari katika Upasuaji, akiwa mwanafunzi wa kimataifa.

Chama cha madaktari wa upasuaji nchini Uganda kimetoa risala za rambirambi kwenye akaunti zao za Twitter.

Mapema wiki hii, wizara ya afya ilisema kuwa wahudumu sita wa afya walipimwa na kukutwa na virusi vya Ebola. Inasemekana wengine waligusana na muathiriwa wa kwanza wa ebola

Wahudumu wengi wa afya walioshughulikia kesi ya kwanza walikuwa wanafunzi. Baadaye walitangaza kuwa walikuwa kwenye mgomo, wakitaja ukosefu wa vifaa vya kujikinga na marupurupu yakujiweka hatarini..

Siku ya Ijumaa, wizara ilitangaza kuwa mlipuko wa Ebola ulikuwa umeenea hadi wilaya ya nne.

Takwimu rasmi zinaonyesha kuwa jumla ya kesi zilizothibitishwa zimefikia thelathini na tano, na vifo vinane.

Watu wawili hadi sasa wamepona ugonjwa huo wa virusi, kulingana na mamlaka ya afya.

Rais Yoweri Museveni amefutilia mbali kufungiwa kwa maeneo yaliyoathiriwa.

Mlipuko wa Ebola nchini Uganda unahusisha aina adimu ya virusi vya Sudan ambayo hakuna chanjo yake.