Viongozi wa mapinduzi nchini Burkina Faso wawataka raia kuwa na utulivu

Wanasema hali imedhibitiwa na utaratibu huo unarejeshwa taratibu.

Image: BBC

Viongozi wa mapinduzi ya Ijumaa nchini Burkina Faso wametoa taarifa kwenye televisheni ya taifa, wakitoa wito wa utulivu na kuwataka waandamanaji kusitisha mashambulizi dhidi ya ubalozi wa Ufaransa na kambi ya kijeshi.

Wanasema hali imedhibitiwa na utaratibu huo unarejeshwa taratibu.

Waandamanaji wamekuwa wakilenga ubalozi wa Ufaransa mjini Ouagadougou kufuatia taarifa ya Junta siku ya Jumamosi, wakidai kuwa kiongozi wa nchi hiyo aliyeondolewa madarakani, Paul-Henri Damiba alikuwa ametafuta hifadhi katika kambi ya kijeshi ya Ufaransa ili kufanya shambulio la kukabiliana.

Ripoti kutoka Ouagadougou zinaonesha baadhi ya wafanyabiashara wa Ufaransa na wahamiaji pia wamelengwa na waharibifu.