Nguo ya jeans ya miaka 143 yauzwa shilingi milioni 9.2

Jeans hii pia iko kwenye hali nzuri na ya kuvaliwa.

Muhtasari

• Kwenye mnada huo vazi hili lilianza kung''ang'aniwa kuuzwa kwa shilingi milioni 3.3 hadi mshindi kupatikana wa shilingi 9.2.

Vazi la kizamani la mika 142 lauzwa kwa shiringi milioni 9.2
Vazi la kizamani la mika 142 lauzwa kwa shiringi milioni 9.2
Image: INSTAGRAM// Lessiswore

Wakaazi katika jimbo la New Mexico nchini Marekani walishangaza ulimwengu baada ya kuweka historia baada ya kuuza jeans kukuu kwa kima cha shilingi milioni 9.2.

Vazi hili linaaminika kuwa ni la zamani sana na limedumu kwa zaidi ya miaka 142, kutokana na ripoti katika Wall Street Journal.

Kwenye mnada huo vazi hili lilianza kung''ang'aniwa kuuzwa kwa shilingi milioni 3.3 hadi mshindi kupatikana wa shilingi 9.2.

Kulingana na Jeans hiyo ilikuwa na chapa ya Levi Strauss & Collection ambayo ni kampuni ya nguo iliyoanzishwa mwaka wa 1853.

Inaaminika halingeuzwa kwa bei ya chini kwani thamani yake ni kama ya dhababu.

Kilichofanya nguo hiyo kuwa na thamani ya juu ni kwamba ilikuwa asili kutoka miaka ya 1880, ilipatikana kwenye shimo la kuchimba madini.

Vazi hili halikufaa kukaa muda huo wote bila kuchanika wala kuwa chafu ndio maana gharama ya kuinunua ikawa juu zaidi.

Vazi hili lilinunuliwa na muuza nguo Mjini humo anayefahamika kama Kyle Haupert wakiwa na Zip Stevenson. Wawili hao walilipa dola 87,400  kwa jumla, " kulingana na maelezo kwenye video.