Masista walima bangi wafanya maombi ili kupata faida ya bangi wanayolima

Wanawake hawa ni "Masista wa eneo hilo," wanaojulikana zaidi kama Watawa wa bangi.

Mtawa Kate (kushoto) akiwa na wenzake kufanya maombi
Image: BBC

Kaunti ya Merced iko katikati ya Bonde la California. Kwa kadiri jicho linavyoweza kuona, kuna safu zinazofanana za mazao, pamoja na banda la muda la shamba au nyumba ya familia.

Kwa nje moja ya nyumba hizi inaonekana isiyo na hadhi. Hakuna jambo lisilo la kawaida kuhusu jengo hilo au ardhi inayolizunguka, isipokuwa kuna kikundi kidogo cha wanawake, wamevalia vitambaa vyeupe kichwani, kuchoma uvumba, na kuimba nyimbo huku wakitembea kwa hatua kubariki mimea yao ya bangi.

Wanawake hawa ni "Masista wa eneo hilo," wanaojulikana zaidi kama Watawa wa bangi.

Wakiongozwa na Mtawa Kate, wanawake hao ni wanachama wa kundi linalojiita watawa wanaojitambulisha kama watetezi wa haki za wanawake, lakini muhimu zaidi, ni wafanyabiashara.

Hawawakilishi dini rasmi. "Nilichagua tasnia ambayo imeharibika," Dada Kate anasema. "

California ni eneo linalojulikana kwa uzalishaji wa bangi. Ilikuwa jimbo la kwanza kuhalalisha bangi kwa ajili ya matibabu mnamo 1996, na matumizi ya burudani yamekuwa halali tangu 2016.

Sheria ya jimbo hilo, hata hivyo, imejaa mianya ya udhibiti, ambayo ina maana kwamba uhalali wa kilimo cha bangi hutofautiana kati ya kaunti na kaunti na jiji moja na jiji lingine.

Kwa hivyo ingawa ni halali kutumia bangi katika jimbo hilo, karibu theluthi mbili ya miji ya California imepiga marufuku biashara ya bangi, na mingine ikifanya kuwa ngumu sana kupata vibali vya kuzalisha zao hilo.

Hii ina maana kwamba kwa Masista ama watawa hawa, hulima mimea yao 60 nje, hapa katika Kaunti ya Merced, haingii ndani ya sheria.

“Polisi wanajua hilo, waliniruhusu tu nifanye hivi,” anakiri Kate. "Lakini kwa kweli hakuna sababu ya wao kuniruhusu.

"Wangeweza kunifungia kwa sasa kwa sababu ni haramu kulima bangi katika kaunti hii. "Lakini nadhani wanajua tutapinga tu sheria na kuifanya ibadilishwe katika kaunti… Na nadhani wanajua itakuwa vita ambayo hawataki kujiingiza."

Wanazalisha na kuuza dawa zao zote zinazotengenezwa kwa bangi, biashara ambayo kabla ya janga la Covid_19 ilikuwa ikiwaingizia dola $1.2m kwa mwaka (£1m).

Licha ya kuombea, na kubariki kila uzalishaji wanaoufanua, sasa wanaingiza nusu tu ya pesa hiyo. Kuuza kupitia zahanati kunaweza kuwasaidia kujijenga upya, lakini hiyo ingemaanisha kukabiliana na kanuni zaidi, na kodi kubwa zaidi.

Maelezo ya picha,

Joel Rodriguez analalamikia kodi kubwa kuwaondoa wengi kufanya biashara ya bangi kihalali

Maili ishirini katikati mwa jiji la Merced, Joel Rodriguez, ambaye anaendesha duka la kuuza bangi, anafanya kazi hiyo kihalali.

Walakini, California imeweka ushuru mwingi kwenye mnyororo wa usambazaji wa bangi, kitu ambacho Bw Rodrigez anasema kinawafanya watu kufanya shughuli hizo kwa kificho na kwa kukwepa kisheria.

Yeye ni mmoja wa wafanyabiashara wengi wa bangi huko California ambao wanalalamika kwa kukandamizwa na ushuru na gharama kubwa za uendeshaji.

"Hatuwezi kupuuza hilo (gharama za juu za ushuru na kodi) na yote yanaingia kwenye gharama ya mwisho kwa mteja."

Ada ya awali ya maombi ya leseni ya kuuza bidha za bangi za rejareja huko California ni $1,000

Maelezo ya picha,

Ruben Chavez wa Idara ya Polisi anasema mapato yatokanayo na bangi yanaweza kusaidia kupambana na wafanyabiashara wa bangi wasiofuata sheria

Kuna wito wa kuikumbatia biashara halali.

"Tunahitaji kuifanya iwe rahisi kidogo kwa wale watu ambao wanaifanya kihalali," anasema Chifu Ruben Chavez wa Idara ya Polisi ya Gustine katika eneo hilo. "Wafanye iwe rahisi kuwa na uwezo wa kuzalisha bidhaa na si lazima kupitia milolongo mingi."

Kufikia sasa na mwaka huu, California imeingiza karibu dola milioni 580 kama mapato ya ushuru na Chifu Ruben anaamini kuwa kurahisisha kanuni kunaweza kusababisha kuongezeka zaidi kwa mapato kwa jiji lake na kusaidia juhudi za idara yake katika kutokomeza biashara hiyo haramu.

"Rasilimali zetu zinapungua," anasema. "Lakini kama tunaweza kupata mapato, usaidizi fulani, sio tu kutoka kwa serikali, labda kutoka kwa Shirikisho la Vyama vya Misitu kuwafuata wale watu ambao wanafanya kinyume cha sheria ... Ukizuia wakulima haramu, na shughuli haramu zaidi, nadhani zile halali, zitaongeza mapato zaidi."

Mbinu hiyo ingewanufaisha wakulima kama Watawa wa bangi, Kate anasema.

"Ukweli ni kwamba, ningependa waturuhusu, kwa sababu hiyo itakuwa ushindi mkubwa. Na kwa sababu tunaamini katika kulipa kodi."