Mfahamu jamaa ambaye mlo wake ni chuma,glasi,wembe,misumari

Iliripotiwa kuwa Lotito anauwezo wa kula gramu 900 za chuma kwa siku.

Muhtasari

• Kufikia mwaka wa 1997, alikuwa amekula karibu tani tisa za chuma.

Image: INSTAGRAM//Guinness Book of World Records

Mwanamume mmoja Mfaransa aliacha dunia nzima ikisemezana baada ya kuingia kwenye vitabu vya rekodi za Guinness kutokana na tabia yake ya kula chuma kama chakula chake.

Jamaa huyo anayefahamika kama Michel Lotito aliwekwa kwenye Guinness Book of Records baada ya kusemekana kuwa alikuwa akila chuma na glasi tangu alipokuwa miaka 9.

Kuta za tumbo la Michel zilikuwa nene mara mbili kuliko za mtu wa kawaida.

Kulingana na chapisho kwenye ukurasa wa Guinness Book of World Records madaktari walimpima Lotito tumboni mwake na mashine ya eksirei na  kusemekana kuwa, mlo wake usio ya kawaida ulitokana na ugonjwa unaoitwa pica.

Ugonjwa huo hufaonya mtu kutamani vyakula ambavyo si vyakula kawaida. Iliripotiwa kuwa Lotito anauwezo wa kula gramu 900 za chuma kwa siku.

Tangu utotoni mwake alikuwa akiwatumbuiza watu jukwani walioshangazwa na tabia yake ya kula vitu vinavyoongopesha kama ile nyembe,misumali,nati,vijiko na vinginevyo.

Tangu Mwaka wa 1966 alikuwa amekula baiskeri 18, toroli 15, seti saba za Runinga, taa za nyumba, ndege ndogo aina ya Cessna na kompyuta.

Kufikia mwaka wa 1997, alikuwa amekula karibu tani tisa za chuma.

Imepita miaka 10 tangu kifo cha Lotito, lakini hakuna aliyeweza kushinda rekodi yake.