Ramaphosa 'kujiondoa' iwapo atashtakiwa kwa kashfa

Mzozo huo unaoitwa "farmgate", unahusu wizi katika shamba la Phala Phala mnamo Februari 2020 na madai ya baadaye.

Muhtasari
  • Wizi huo unadaiwa kufanywa na raia wa Namibia ambao walikula njama na mfanyakazi wa ndani katika shamba hilo
Rais Cyril Ramaphosa
Image: PSCU

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa "atajiuzulu" iwapo atashtakiwa kwa madai ya kuficha wizi katika shamba lake la kibinafsi, kulingana na msemaji wake.

"Iwapo rais atashtakiwa atajiondoa madarakani - ikiwa ni hivyo," msemaji wa rais Vincent Magwenya aliwaambia waandishi wa habari.

Aliongeza: "Lakini kwa hali ilivyo hakuna mashtaka ya jinai dhidi ya rais. Mlichonacho ni msururu wa uchunguzi ambao anashirikiana nao kikamilifu na ataendelea kufanya hivyo."

Mzozo huo unaoitwa "farmgate", unahusu wizi katika shamba la Phala Phala mnamo Februari 2020 na madai ya baadaye.

Wizi huo unadaiwa kufanywa na raia wa Namibia ambao walikula njama na mfanyakazi wa ndani katika shamba hilo.

Rais anatuhumiwa kwa utekaji nyara, utoaji hongo na kutenda kinyume cha sheria kwa madai ya kuidhinisha a kufuatwa kwa washukiwa walioiba takriban $4m (£3.2m) kutoka kwa shamba lake. Anakanusha kosa lolote.