Mbunge wa Rwanda ajiuzulu, 'aacha pombe', na kuomba radhi kwa kuendesha gari akiwa mlevi

Bw Gamariel Mbonimana aliomba msamaha kwa Wanyarwanda na rais, na kuongeza kwamba "ameamua kutokunywa tena pombe".

Muhtasari

• Bw Mbonigaba, hakueleza zaidi kuhusu msamaha wake lakini alithibitisha kwa BBC kwamba ujumbe huo wa Twitter ulikuwa "wangu".

Image: RWANDA PARLIAMENT

Mbunge wa Rwanda ambaye alijiuzulu katika bunge siku ya Jumatatu sasa ameomba msamaha kwa "kuendesha gari akiwa mlevi".

Siku ya Jumatatu, bunge liliidhinisha kujiuzulu kwake kwa "sababu za kibinafsi", ilikuwa siku moja baada ya Rais Paul Kagame kumkosoa mbunge ambaye hakumtaja jina, kwa kuendesha gari akiwa mlevi.

Katika taarifa kwenye Twitter, Bw Gamariel Mbonimana aliomba msamaha kwa Wanyarwanda na rais, na kuongeza kwamba "ameamua kutokunywa tena pombe".

Bw Mbonigaba, hakueleza zaidi kuhusu msamaha wake lakini alithibitisha kwa BBC kwamba ujumbe huo wa Twitter ulikuwa "wangu".

Uendeshaji gari ukiwa mlevu una adhabu ya faini ya faranga 150,000 za Rwanda ($140/£120), lakini jela ya siku tano chini ya ulinzi wa polisi imeongezwa kwa wale wanaokamatwa kwa kesi hiyo.

Katika matamshi yake mwishoni mwa wiki, Bw Kagame alikosoa polisi kwa kutomkamata mbunge huyo kwa sababu ya "kinga yake".

Bw Mbonimana alikuwa mbunge tangu 2018, yeye ni mwanachama wa Liberal Party, chama mshirika wa chama tawala cha Kagame, RPF.

Makamu wa rais wa chama chake Théogène Munyangeyo ameambia shirika la utangazaji la serikali kuwa "hawajawahi kumuona akinywa pombe hapo awali".