Rais Museveni asema sababu kuu kwa nini hawezi kumbusu mke wake hadharani

Rais huyo pia alikashfu vikali makundi yale yanayopigania haki ya wapenzi wa jinsia moja, na kusema hilo haliwezi kutokea nchini Uganda.

Muhtasari

• Museveni alisema kuwa kumbusu mkewe hadharani kunaweza kuwa na madhara makubwa kwa upande wake kisiasa.

rais Museveni na mkewe Janet
rais Museveni na mkewe Janet
Image: Maktaba

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amezua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii baada ya video kuonekana akikashfu vikali mapenzi ya jinsia moja na pia watu kuoneshana mapenzi hadharani kwa kupatiana mabusu.

Kulingana na Museveni, Wafrika wana mila zao na yeye kama Mwafrika halisi kuna mambo mengine hayawezi umuingia kichwani ambayo yanaendekezwa na watu kutoka jamii za ulaya.

Museveni alitolea mfano kwamba katika mila na tamadnuni za Kiafrika, Watu hawafai kubusiana hadharani na iwapo yeye kama rais atambusu mkewe hadharani basi atapoteza kura katika chaguzi zote nchini Uganda.

“Ikiwa ningembusu mke wangu hadharani, ningepoteza uchaguzi wote nchini Uganda. Kwa sababu Waafrika hawaonyeshi yaliyo faragha hadharani. Ukitaka kumbusu unajua anuani ya kumbusu ilipo,” rais Museveni alisema huku umati ukipasua vichekesho.

Rais huyo pia alisema haifai hata kidogo watu wa jinsia moja kusifiwa hadharani kwani hiyo si hali ya maumbile na si matakwa ya Mungu bali ni wale waliotoroka kutoka uhalisia wa ukweli.

“Tunashinikizwa na vikundi vinavyosema kuna njia mbili za maisha. Kuna njia ya kawaida na kuna njia sambamba ya mashoga na wote. Hii sio tafsiri yetu. Mashoga walikuwa hapa muda mrefu uliopita. Nasikia mmoja wao alikuwa chifu, mwingine mfalme. Hawakuuawa. Hawakusifiwa na kupandishwa vyeo. Haikuwekwa wazi kuwa ilikuwa njia ya kawaida,” Museveni alisema.

Mnamo mwaka wa 2014, Rais Museveni alitia saini kuwa sheria mswada unaoelezea kwa kina adhabu kwa mashoga, ikiwa ni pamoja na kifungo cha maisha kwa kufanya mapenzi ya jinsia moja na ndoa za jinsia moja.