• Dawa za kupunguza makali ya virusi sasa yanapatikana kila mahali lakini mafanikio sio sawa.
• Umoja wa Mataifa unasema, huku 76% ya watu wazima kwa ujumla walipokea dawa hizo -antiretrovirals katika mwaka 2021, ni 52% pekee ya watoto (wa miaka kuanzia 0-14 ) waliopata tiba hiyo.
Maafisa wa afya walifahamu kwa mara ya kwanza kuhusu Ukimwi katika majira ya kiangazi mwaka wa 1981.
Katika miaka ya 1980, Kwa mtu kupatikana na Ukwimwi ilionekana kama 'waranti ya kifo' lakini kutokana na maendeleo na sayansi ya matibabu, inawezekana sasa kwa kiasi kikubwa kwa wagonjwa wanaoishi na virusi vya HIV kuishi maisha ya afya.
Lakini Umoja wa Mataifa unasema kwamba watoto wanaoishi na virusi vya HIV hawapati msaada unaofaa. Tulizungumza na vijana watatu wanaoishi na HIV.
"Dunia inaendelea kushindwa kuwasaidia watoto katika kukabiliana na Ukimwi. Maambukizi mapya miongoni mwa watoto yanaweza kuzuiwa lakini bado watoto 160,000 walipata maambukizi mapya mwaka 2021," anasema Fodé Simaga, Mkurugenzi wa , Global Practice Science, Systems na Services for All, UNAIDS.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa , zaidi ya watu milioni wameambukizwa tangu mwanzoni mwa janga na zaidi ya watu milioni 40 walikufa kutokana na magonjwa yanayohusiana na Ukimwi.
Ikilinganishwa na siku za mwanzo wa janga, dawa za kupunguza makali ya virusi sasa zinapatikana kila mahali lakini mafanikio sio sawa.
Umoja wa Mataifa unasema, huku 76% ya watu wazima kwa ujumla walipokea madawa hayo -antiretrovirals katika mwaka 2021, ni 52% pekee ya watoto (wa miaka kuanzia 0-14 ) waliopata tiba hiyo.
BBC ilizungumza na vijana watatu kutoka nchi tofauti , wanaoishi na virusi vya HIV.
'Mtoto wangu hatazaliwa na HIV'
Martha Clara Nakato ni msichana Mganda mwenye umri wa miaka 26 anayeishi mjini Kampala. Alipatikana na Ukimwi alipokuwa na umri wa miaka 14 pekee.
Image: MARTHA CLARA NAKATO
Kaka yake ambaye ni pacha wake alishiriki ngono bila kinga na alikuwa na wasiwasi. Walikwenda kwenye kituo cha kupima HIV wakiwa pamoja. Kwasababu kupima ugonjwa ilikuwa ni bure, pia alipima. Huku kaka yake alipatikana bila virusi Martha alipatwa na virusi
"Ninakumbu kaka, pacha wangu akinigeukia na kuniambia , 'Hey, ulifanya ngono?' Nilisema, hapana sijui hii imetoka wapi '.."
Mama yake Martha alifariki wakati Martha alipokuwa na umri wa miaka mitano. Alilelewa na baba yake. Wote pamoja walikuwa wanaishi na virusi vya HIV.
Kati ya ndugu zake wanane alikuwa ni yeye pekee aliyeambukizwa na wazazi wake.
"Kusema ukweli sikuona haja ya kuishi. Vyombo vya habari wakati ule vilikuwa vikitangaza taarifa zinazowanyanyapaa watu. Ulaya HIV ilihusishwa na watu wanaotumia madawa ya kulevya.
Ulaya ilihusishwa na ngono. Ilinusumbua sana. Nilitaka kujiua."
Martha alipata faraja katika kuwasaidia vijana wengine wadogo wenye uzoefu sawa na wake na kujiunga na kikundi cha usaidizi cha HIV.
Martha pia anafanya kampeni kuhusu haki za afya hususan kuhusu afya ya ngono na uzazi
"Wakati unapofanya ngono ya kawaida au kwa usiku mmoja unafurahia wakati kwa usalama. Tumia tu mipira ya kinga ," anashauri.
Martha anatambua ugumu wa kuwa muwazi kuhusu HIV. Lakini hamfichi lolote mpenzi wake.
"Nina uhakika wa asilimia 101 kuwa nitakuwa mama siku moja na mtoto nitakayemzaa, hatakuwa na HIV. Ninasema hilo kwa matumaini yote niliyonayo moyoni mwangu, kwasababu nimekuwa nikipata dawa zenye ufanisi sana ."
'Sitegemei mengi kutoka kwa jamii'
Lulu Mangang, ni mwanaume aliyebadili jinsia mwenye umri wa miaka 23 na mwanaharakati wa kampeni dhidi ya Ukimwi mwenye makao yake katika Imphal, Kaskazini Mashariki mwa India.
Alisomea masomo ya baiolojia ya wanyama (zoology) na sasa anapanga kufanya masomo ya uzamili ya bayokemia( biochemistry). "Ningependa kufanya utafiti kuhusu ufanisi wa madawa ya HIV," anasema.
Lulu alizaliwa katika mji wa Delhi mwaka 1999 katika familia masikini. Bada ya kifo cha baba yake mwaka 2002, alilelewa na mjomba wake. Anasema "alipatikana na HIV akiwana umri wa miaka 6 au 7."
"Sikujua nifanye nini. Nilikuwa mwenye hasira na masikitiko. Ulikuwa ni mchanganyiko wa hisia. Sijui ni nani wa kumlaumu. Nilijikasirikia mwenyewe pia na kujilaani ."
"Nilizungumza na mama yangu na akaniambia nilipata HIV kutoka kwake ," Lulu anakumbuka
Mama yake alimpeleka katika kikundi cha watoto walioapatwa na maambukizi ya HIV ambacho kilimsaidia Lulu kupata marafiki lakini pia alikabiliwa na ubaguzi.
"Wakati nilipokuwa ninacheza na mtoto mmoja ghafla nilitaja hali yangu na akaniambia nisimsogelee au kucheza naye. Halafu tuligombana sana ambapo sote tulimia sana."
Kadri alivyokua, alijifunza jinsi ya kuishi na changamoto.
Sitegemei mengi kutoka kwa jamii". Tuko tofauti na sote tuna fikra tofauti."
"Baadhi wanaweza kuniona kama ninavyojiona mwenyewe. Baadhi hawawezi."
Lulu anasema hakuwahi kupata matatizo wakati anapotafuta matibabu kutokana na jinsia yake. Kwa miaka mitatu iliyopita anafanya kazi kama mwanaharakati katika shirika lisilo la serikali ambalo linamuwezesha kufanya kazi na vijana wenye maambukizi ya HIV.
Lulu anaamini kuna haja ya kuongeza uelewa ili kuzua ubaguzi "Kutokana na ukosefu wa kutojiamini na ukosefu wa taarifa watu wengi wanakabiliwa na ubaguzi na kunyanyaswa."
"Niliamua kuwa muwazi kuhusu hali yangu sio kwasababu inakubalika kiurahisi hapa katika jimbo langu (Manipur).
Mbinu yake ilipokelewa vyema, vijana wengi wanawasiliana naye ili kupata ushauri na usaidizi.
UKIMWI katika namba
- Watu milioni 38.4 kote duniani walikuwa wanaishi na HIV katika mwaka 2021
- Watu milioni 1. walipatwa na maambukizi mapya ya HIV mwaka 2021 Watu 650 000 [walikufa kutokana magonjwa yanayohusiana na Ukimwi katika mwaka 2021.
- Idadi hiyo inajumuisha watoto na vijana wenye umri wa kubarehe kote duniani wapatao 110,000 (wenye umri kati ya 0-19 )
- Idadi ya vijana wadogo wanaoishi na HIV wanafikia hadi milioni 2.7 Watoto na vijana wadogo ni 7 % ya watu walioambukizwa virusi vya HIV lakini walichukua 17 % ya vifo na 21 % ya maambukizi mapya katika 2021.
- Watu milioni 84.2 ndi waliopatwa na maambukizi ya HIV tangu janga hilo lilipoanza na milioni 40.1 kati yao wamekwishafariki kutokana na magonjwa yanayohusiana na Ukimwi
Chanzo : UN AIDS na Unicef
'Nitafichua hali yangu ya HIV wakati nitakapokuwa tayari
Ayana, ni mwanafunzi wa chuo kikuu mwenye umri wa miaka 18 aliyezaliwa katika Osh, Kyrgyzstan. Kwa sasa anaishi katika mji mkuu Bishkek.
"Tangu nilipojitambua, ninaishi na virusi ," aliiambia BBC.
Katika mwaka 2006-2007, watoto 391 walipata maambukizi ya HIV, waliyoambukizwa wakati walipokuwa wakipata matibabu hospitali akiwemo Ayana, UNAIDS inasema.
Mama yake Ayana alihudhuria msururu wa semina ambazo zilimsaidia kumlea binti yake bila hofu.
Wakati alipokuwa na umri wa kubalehe Ayana alijiunga na makundi ya usaidizi ya HIV.
"Tunasaidiana. Pia tunazungumzia kuhusu fursa ," anasema.
Kinyume na Ayana wasichana wengine hawanywi dawa kila siku, lakini anajaribu kuwasaidia.
"Nina rafiki ambaye hakutaka kumeza vidonge. Tulibuni maneneo ya siri ya kuwasiliana. Wakati ninapotaka kuwakumbusha rafiki zangu kuhsuu dawa, nitauliza ulikumbuka kumwagilia maji maua?"
Ayana amefichua hali yake tu kwa familia yake na ndugu wa karibu.
"Siku moja nitajitokeza wazi, lakini sitafanya hivyo kwa ajili ya wazazi wangu au kwa ajili ya mtu fulani. Nitafanya hivyo wakati niko tayari ."
Ayana anasema anafahamu ugumu unaowakabilia marafiki ambao hali yao ilijulikana bila wao kuitangaza.
"Unyanyapaa na ubaguzi bado upo. Hivi karibuni daftari la kumbukumbu la rafiki yangu lilichukuliwa na mwanafunzi mwenzake na wakabaini hali yake ya HIV. Taarifa ilisambazwa sana na akakabiliwa na uonevu na hatimaye aliihama shule."
Ayana amepata nafasi katika chuo kikuu na ana matumaini ya kuwa mwandishi wa habari katika kipindi cha miaka michache. Katika muda ambao hajatingwa na kazi huandika hadithi na ana matumaini kuwa atakuwa na maisha mazuri yajayo.
"maisha ni kama maji yanayotiririka. Kila kitu kilichotokea kimenifanya niwe nilivyo leo. Ninataka kuendelea kuishi katika maisha haya na nione yananipeleka wapi ."