Pelé kuzikwa kwenye ghorofa ya 9 ya makaburi ili 'aone' uwanja uliompa umaarufu

Pelé alichagua kumiliki ghorofa ya tisa ya jengo hilo mwaka wa 2003, kama njia moja ya kumuenzi baba yake aliyekuwa akivaa jezi namba 9 wakati akicheza.

Muhtasari

• Jumba hilo la makaburi lina ghorofa 14 lakini Pele alichagua kuzikwa katika ghorofa ya 9.

• Mashabiki wake wanaojitolea wanaamini kwamba Pele daima ataweza "kuona" uwanja wake wa soka kwa milele.

Mbeazil Pele atazikwa katika kaburi la ghorofa
Mbeazil Pele atazikwa katika kaburi la ghorofa
Image: Hisani

Mfalame na muasisis wa soka la kisasa kutoka Brazil, mkongwe Pele aliyefariki wiki iliyopita atazikwa katika ghorofa ya 9 ya makaburi ya familia yenye ghorofa 14.

Kulingana na taarifa kutoka Brazil, Pele alichagua kuzikwa katika ghorofa ya 9 ili kuendelea kutazama uwanja ambao ulimpa umaarufu katika mechi za ligi ya Brazil ambao ni uwanja wa timu ya Santos aliyoitumikia kwa muda mrefu na kupata umaarufu mkubwa maishani.

Mashabiki wake wanaojitolea wanaamini kwamba Pele daima ataweza "kuona" uwanja wake wa soka kwa milele.

Nyota huyo wa Brazil - mwanamume pekee katika historia kuwahi kushinda vikombe vitatu vya Dunia - alitumia muda mwingi kuchagua sehemu yake ya mwisho ya 'kuzikwa'.

Pele atazikwa Jumanne, huku shughuli za mazishi ikielezwa zitafanana na zile za Malkia. Uwanja wa Vila Belmiro, unaotumiwa na Santos FC, timu ambayo Pele alitumikia kwa sehemu kubwa ya maisha ya mpira. Uwanja huo ndiyo utatumika kwenye shughuli za mazishi Jumatatu na Jumanne. Santos historia yake haielezewi bila ya kumtaja Pele na ndiyo maana wamelichukua jukumu zima la mazishi yake.

Nyota mashuhuri wa kandanda wa Brazil atalala katikati ya uwanja wa Santos kwa saa 24, huku maelfu wakitarajiwa kutembelea jeneza lake kutoa heshima zao za mwisho.

Kisha itaonyeshwa barabarani hadi Ecumenical Necropolis Memorial, ikisimama kwa muda mfupi katika nyumba ya mama yake aliyeko kitandani.

Pelé alichagua kumiliki orofa ya tisa ya jengo hilo mwaka wa 2003, kama njia moja ya kumuenzi baba yake aliyekuwa akivaa jezi namba 9 wakati akicheza.