Mchezaji wa Manchester City Benjamin Mendy akutwa bila hatia ya makosa sita ya ubakaji

Louis Saha Matturie, 41, pia alipatikana bila hatia ya makosa matatu ya ubakaji.

Muhtasari
  • Uamuzi huo kwa kauli moja ulitolewa Jumatano na wanaume saba na wanawake wanne mmoja alikuwa ameachiliwa mapema kwa sababu za matibabu
BENJAMIN MENDY
Image: REUTERS

Mchezaji wa Manchester City Benjamin Mendy amepatikana bila hatia ya makosa sita ya ubakaji na moja la unyanyasaji wa kingono.

Majaji hawakuweza kufikia uamuzi kuhusu shtaka moja la ubakaji na lile la kujaribu kubaka, kufuatia kesi iliyodumu kwa miezi sita katika Mahakama ya Chester Crown.

Upande wa mashtaka ulitaka kusikilizwa upya kwa makosa hayo

Louis Saha Matturie, 41, pia alipatikana bila hatia ya makosa matatu ya ubakaji.

Majaji walishindwa kutoa uamuzi kwa makosa matatu ya ubakaji na makosa matatu ya unyanyasaji wa kingono dhidi yake.

Bw Mendy na rafiki yake Bw Matturie walikuwa wameshtakiwa kwa ubakaji na wanawake katika nyumba ya mchezaji huyo huko Prestbury, Cheshire, na katika gorofa ya Manchester.

Waendesha mashtaka waliiambia mahakama kuwa Bw Mendy alikuwa "mwindaji" ambaye aligeuza harakati za kuwatafuta wanawake kufanya ngono kuwa mchezo.

Bw Mendy alifunika uso wake kwa mikono yote miwili huku jaji wa mahakama akirudia "hana hatia" kwa makosa sita, ambayo yalihusiana na wasichana wanne au vijana.

Uamuzi huo kwa kauli moja ulitolewa Jumatano na wanaume saba na wanawake wanne mmoja alikuwa ameachiliwa mapema kwa sababu za matibabu.

Lakini baada ya siku 14 za mashauriano, majaji hawakuweza kufikia uamuzi kuhusu madai dhidi ya Bw Mendy ya kumbaka mwanamke, 29, mwaka wa 2018 na madai ya kumbaka mwanamke mwingine, 24, Oktoba 2020.

Jaji Everett siku ya Ijumaa alimaliza kesi hiyo. Wanaume hao wawili walikuwa wameshtakiwa tangu Agosti 10, wakituhumiwa kwa makosa mengi ya ngono na wanawake 13.

Matthew Conway, akiendesha mashtaka, alisema mwendesha mashtaka alitaka kusilikizwa upya kwa makosa ambayo majaji hawakuweza kufikia uamuzi. Alisem.

"Upande wa mashtaka umefanya uamuzi. Tumefanya uamuzi leo, ambao ni kuendelea na mashtaka haya katika kesi mbili tofauti na tunatafuta leo usimamizi wa kesi ya muda." Taarifa kutoka Manchester City ilisema.

"Kwa kuzingatia kuwa kuna mambo ya wazi kuhusiana na kesi hii, klabu haiko katika nafasi ya kutoa maoni zaidi kwa sasa."

Madai na kesi zimekuwa "mbaya kabisa" kwa Bw Mendy, mahakama ilielezwa, huku maisha yake katika soka yakiwa "yameisha" kwani "hangekwepa" shutuma hizo.