BBC watoa tamko baada ya Sauti ya kushiriki mapenzi kusikika wakati wa mechi ya Liverpool na Wolves

Mchambuzi alisema kuwa sauti hiyo ilikuwa inatoka kwa simu ambayo ilikuwa imewekwa nyuma ya studio ikitoa sauti ya watu kushiriki mapenzi.

Muhtasari

• "Tunaomba radhi kwa watazamaji wowote walioudhika wakati wa matangazo ya moja kwa moja ya kandanda jioni hii," BBC ilisema.

Simu iliyokuwa ikitoa sauti hiyo
Simu iliyokuwa ikitoa sauti hiyo
Image: Twitter,

BBC imeomba msamaha baada ya kelele za kushiriki mapenzi kukatiza matangazo ya moja kwa moja ya televisheni ya Kombe la FA baina ya Liverpool na Wolves Jumanne usiku.

Sauti hizo zilisikika wakati mtangazaji Gary Lineker akiwasilisha mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya tatu.

Mchambuzi huyo wa kandanda baadaye alichapisha picha ya simu ya rununu aliyosema "ilirekodiwa nyuma ya seti"

Baada ya sauti hiyo kusikiza na wengi wa waliokuwa wakifuatilia uchambuzi wake, shirika la BBC lililazimika kutoa tamko rasmi la kuomba radhi.

"Tunaomba radhi kwa watazamaji wowote walioudhika wakati wa matangazo ya moja kwa moja ya kandanda jioni hii," BBC ilisema.

Lineker alijaribu kuchekelea tukio hilo alipokuwa akiwasilisha kipindi hicho katika studio kwenye Uwanja wa Wolverhampton wa Molineux pamoja na wachambuzi Paul Ince na Danny Murphy.

Alipomkataza mwenzake na mshambuliaji mwenzake wa zamani wa England Alan Shearer kwenye uwanja wa maoni, alisema: "Nafikiri kuna mtu anatuma kitu kwenye simu ya mtu. Na sijui kama mliisikia nyumbani,”

Baadaye, mtangazaji huyo alisema kuwa simu ilikuwa imenaswa nyuma ya kiti cha studio kama mizaha ambayo ilienda vibaya na hata alionesha picha ya kisimu hicho cha mkononi kikiwa kimebandikizwa nyuma ya kiti.

“Kweli, tulipata hii imefungwa nyuma ya seti. Hujuma inavyoendelea ilikuwa ya kufurahisha sana,” alisema kupitia Twitter yake.

GiveMe Sport baadae waliripoti kuwa mtu anayedaiwa kuwa nyuma ya mzaha huo ambao ulichoma picha vibaya mno tayari ameshatambuliwa na kukamatwa.

Sasa inasubiriwa kuonekana hi hatua gani za kisheria zitakazochukuliwa dhidi yake.

Katika mechi hiyo ya kufuzu awamu ya 4 ya kombe la FA, Wolves walishindwa nyumbani kwa kufungwa bao moja kapa na mchezaji Elliot wa Liverpool.

Wiki jana, Liverpool na Wolves walimaliza kwa sare katika uwanja wa Anfield, kupelekea marudio ya mechi hiyo ili kupata mshindi.