Maaskofu wa Kanisa la England wakataa kuunga mkono ndoa za watu wa jinsia moja

Ndoa ya watu wa jinsia moja imekuwa halali England na Wales tangu mwaka 2013.

Muhtasari

• Maaskofu wa kanisa la England walikutana Jumanne kukamilisha mapendekezo yao baada ya miaka mitano ya kufanya mashauriano.

• Ndoa ya watu wa jinsia moja imekuwa halali kisheria katika England na Wales tangu mwaka 2013.

Kanisa la England limekuwa likijadili suala hilo kwa miaka mingi – msimamo wake huenda ukawa kinyume na kanisa la Kiepiskopi la Uskochi na Kanisa la Uskochi
Kanisa la England limekuwa likijadili suala hilo kwa miaka mingi – msimamo wake huenda ukawa kinyume na kanisa la Kiepiskopi la Uskochi na Kanisa la Uskochi
Image: REUTERS

Maaskofu wamekataa kuunga mkono mabadiliko katika mafundisho ili kuwaruhusu makasisi  kuwafungisha ndoa watu wa jinsia moja, vyanzo vya habari vimeiambia BBC News.

 Maaskofu wa kanisa la England walikutana Jumanne kukamilisha mapendekezo yao baada ya miaka mitano ya kufanya mashauriano na mjadala  kuhusu msimamo wa kanisa kuhusu uwezo wa jinsia wa kingono.

Pendekezo lao litajadiliwa baada ya badara la kanisa ambalo ni sawa na bunge  - au  Sinodi kuu- mwezi ujao.    

BBC ilizungumza na maaskofu kadhaa waliokuwepo katika mkutano huo waliosema kuwa mafundisho ya Kanisa kwamba ndoa takatifu ni baina ya mwanamume na mwanamke hayatabadilika na hilo halitapigiwa kura.    

 Hii inakuja baada ya miaka ya mjadala kuhusu suala hili  

Ndoa ya watu wa jinsia moja imekuwa halali kisheria katika England na Wales tangu mwaka 2013. Lakini wakati sheria ilipobadilika, kanisa halikubadili mafindisho yake. 

 Katika mwaka 2017, Kanisa la England (Church of England) lilianza kuongeza kipindi cha mashauriano yanayoitwa    'Kuishi katika Mapenzi na Imani'.

Mwezi Nonvemba mwaka jana, Askofu wa Oxford  alikuwa askofu wa ngazi ya juu zaidi wa  Kanisa la England kuunga mkono hadharani mabadiliko katika mafunzo ya Kanisa. Ingawa maaskofu wachache walimuunga mkono, walisalia kuwa wachache miongoni mwa Maaskofu wengi waliopinga mabadiliko hayo.  -

Kukataliwa kwa pendekezo la kupigia kura suala la kuruhusu watu wa jinsia moja kuoana linatarajiwa kuwakasirisha wanakampeni wanaotaka mabadiliko ndani ya Kanisa. 

 Baadhi tayari wameiambia BBC kuwa wataomba ifanyike Sinodi nyingine ili kuondoa mapendekezo ya maaskofu mwezi ujao. 

'Maombi ya baraka ya Mungu'

Uamuzi wa maaskofu unaliweka Kansia la England katika msimamo unaokinzana na uke wa Kanisa la  Kianglikana la  Scotland, Kanisa la Kiepiskopi la Uskochi, na Kanisa la Kipresbyterian la Uskochi, ambayo yote yanaruhusu harusi za watu wa jinsia moja.

 Kanisa la kianglikana la Wales limetoa idhini ya huduma ya kuwapatia baraka wenzi wa jinsia moja lakini haliruhusu  ndoa ya jinsia moja kanisani. 

 Maskofu wa Kiingereza watapendekeza kwamba ‘’maombi kwa baraka za Mungu’’ kwa ajili ya wenzi wanaofunga ndoa za kiserikali yaidhinishwe, wanasema wataalamu wa BBC.

Waraka tata wa kanisa kuanzia mwaka 1991 ambao unasema kuwa kasisi katika mahusiano ya  kimapenzi ya jinsia moja ni lazima aendelee kuwa mseja  utafutiliwa mbali.

Na Kanisa pia litaomba msamaha kwa jinsi lilivyowatenga watu wanaoshiriki mapenzi ya  jinsia moja  na walioamua kubadili utambulisho wa jinsia yao - LGBT+ , BBC iliambiwa na maakofu kadhaa.

Mmoja wa maaskofu mwenye fikra huria ambaye alishiriki mkutano  alisema kuwa ‘’ kumekuwa na mafanikio makubwa’’ 

"Ni mageuzi," alisema. " Sio mwisho wa barabara."

Askofu mhafidhina alisema: "Tunakuwa wakweli kuhusu ukweli kwamba sisi sio watu wenye akili zinazofanana katika suala hili. Lakini hatutakata tamaa ya kutembea pamoja."

'Kukatishwa tamaa sana'


Charlie Bell (kulia ) na mwenza wake Piotr walisema kuwa wataendelea kuendesha kampeni ili Kanisa libadilishe mafundisho yake kuhusu ndoa.
Charlie Bell (kulia ) na mwenza wake Piotr walisema kuwa wataendelea kuendesha kampeni ili Kanisa libadilishe mafundisho yake kuhusu ndoa.
Image: CHARLIE BELL

Charlie Bell, 33, na mwenzake Piotr Baczyk, 27, wanaishi kusini mashariki mwa London, ambako Charlie ni kasisi. Wamekuwa wakisubiri kuoana hadi kanisa litakaporuhusu wapenzi wa jinsia moja kufanya harusi kanisani. 

Anasema walihisi "kukatishwa tamaa sana" kwamba maaskofu hawakupendekeza kura kuhusu ndoa za  jinsia moja.   

" Inawaacha wenzi wa jinsia moja katika utata kidogo na pia kama raia wa daraja la pili," aliiambia BBC News.

"Bado tunawaambia wenzi wa jinsia moja kwamba mahusiano yao ni ya kiwango cha chini baina ya watu wa jinsia tofauti ."

Hata hivyo, anasema tutaendelea kukampeni ili Kanisa libadilishe mafundisho yake kuhusu wenzi wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja. 

Alisema: "hii haijafika mwisho. Kama maaskofu wanafikiri hili litatatua hali ya sasa wamedanganyika sana."