Shabiki wa Tottenham aliyempiga kipa wa Arsenal mashakani

Ramsdale alikuwa kiungo muhimu sana wakati Arsenal iliposhinda derby ya London kaskazini 2-0.

Muhtasari
  • Joseph Watts, 35, kutoka Hackney, anatarajiwa kufika katika Mahakama ya Highbury mnamo tarehe 17 Februari
Image: BBC

Mwanaume mmoja ameshtakiwa kwa kosa la kumpiga mlinda mlango wa Arsenal Aaron Ramsdale baada ya mechi ya Jumapili ugenini dhidi ya Tottenham.

Polisi wa Metropolitan walithibitisha kuwa mtu huyo anakabiliwa na mashtaka ya kushambulia kwa kumpiga, kwenda kwenye eneo lililo karibu na eneo la kuchezea na kurusha kitu .

Joseph Watts, 35, kutoka Hackney, anatarajiwa kufika katika Mahakama ya Highbury mnamo tarehe 17 Februari.

Ramsdale alikuwa kiungo muhimu sana wakati Arsenal iliposhinda derby ya London kaskazini 2-0.

Spurs, wenyeji Jumapili, wameisaidia timu ya uchunguzi wa soka ya Met katika maswali yao.

Kisa hicho kililaaniwa na Chama cha Wanasoka wa Kulipwa na Chama cha Soka, huku Tottenham ikisema kuwa shabiki huyo atapigwa marufuku mara moja.