Museveni aonya dhidi ya 'upuuzi' wa wapenzi wa jinsia moja nchini Uganda

Aliongeza kuwa alifurahi kuhudhuria mkutano wa hivi karibuni nchini Marekani ambapo masuala ya haki za wapenzi wa jinsia moja hayakuzungumziwa.

Muhtasari
  • Siku ya Jumatano rais alitaja haki za wapenzi wa jinsia moja kama "upuuzi" wakati wa hotuba aliyoitoa kwenye mahafali ya Chuo cha Kitaifa cha Ulinzi
RAIS WA UGANDA YOWERI MUSEVENI
Image: BBC

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameonya dhidi ya kampeni zinazounga mkono haki za wapenzi wa jinsia moja nchini humo.

Mapenzi ya jinsia moja tayari ni haramu nchini Uganda.

Sheria ilisainiwa mwaka 2014 ambayo inaruhusu kifungo cha maisha kwa watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja na ndoa za watu wa jinsia moja.

Siku ya Jumatano rais alitaja haki za wapenzi wa jinsia moja kama "upuuzi" wakati wa hotuba aliyoitoa kwenye mahafali ya Chuo cha Kitaifa cha Ulinzi.

Aliongeza kuwa alifurahi kuhudhuria mkutano wa hivi karibuni nchini Marekani ambapo masuala ya haki za wapenzi wa jinsia moja hayakuzungumziwa.

Rais alisema: Ujumbe wa Nukuu: Usilete upuuzi wowote hapa... Tulikuwa Washington, na wakati huu Wamarekani walipanga mkutano vizuri kwa sababu hawakuleta masuala haya. Walijikita kwenye biashara, suala ambalo ni zuri. Hawakuleta masuala yoyote kuhusu wapenzi wa jinsia moja . Lakini kama wangeleta hizo mada tungekuwa na matatizo."