Shambulio la anga la Marekani 'laua wanamgambo 30' wa Al-Shabaab Somalia

Hapo awali wanamgambo hao waliwaua wanajeshi saba baada ya kuvamia kambi ya kijeshi huko Galcad.

Muhtasari

•Operesheni hiyo ilifanyika karibu na mji wa Galcad, yapata kilomita 260 (maili 162) kaskazini mashariki mwa mji mkuu Mogadishu.

•Wakati Al Shabaab imesukumwa nje ya Mogadishu na maeneo mengine inaendelea kushambulia malengo ya kijeshi na ya kiraia.

Image: BBC

Shambulio la anga la Marekani lililowasaidia wanajeshi wa serikali nchini Somalia limewaua takribani wanamgambo 30 wa Kiislamu wa al-Shabab, jeshi la Marekani linasema.

Operesheni hiyo ilifanyika karibu na mji wa Galcad, yapata kilomita 260 (maili 162) kaskazini mashariki mwa mji mkuu Mogadishu.

Katika siku chache zilizopita, jeshi la Somalia na wanamgambo wa al-Shabab wamepigana kuudhibiti mji huo.

Mashambulizi ya anga ya Ijumaa yalitokea huku jeshi likishambuliwa na zaidi ya wanamgambo 100, kamandi ya Marekani barani Afrika inasema.

Hapo awali wanamgambo hao waliwaua wanajeshi saba baada ya kuvamia kambi ya kijeshi huko Galcad. Wizara ya Habari ya Somalia ilisema makumi ya wanamgambo hao waliuawa.

Al-Shabab imekuwa ikipambana na serikali kuu ya Somalia tangu mwaka 2006, kwa lengo la kulazimisha utawala wa Kiislamu wenye itikadi kali.

Wakati imesukumwa nje ya Mogadishu na maeneo mengine inaendelea kushambulia malengo ya kijeshi na ya kiraia.

Jumatatu iliyopita serikali ilisema jeshi lake na wanamgambo wa ndani wameuteka mji wa bandari wa Harardhere, ambao umekuwa kituo kikuu cha usambazaji cha al-Shabab tangu 2010.

Katika ripoti yake kuhusu kundi la Galcad linalopigana na Kamandi ya Marekani ya Afrika ilisema magari matatu ya al-Shabab yaliharibiwa na "kamandi hiyo inatathmini kuwa hakuna raia aliyejeruhiwa au kuuawa".

Maelezo hayajathibitishwa. "Vikosi vya Kamandi ya Marekani ya Afrika vitaendelea kutoa mafunzo, kushauri na kuandaa vikosi vya washirika kusaidia kuwapa zana wanazohitaji kuishinda al-Shabab, mtandao mkubwa na hatari zaidi wa al-Qaeda duniani," ilisema taarifa hiyo.

Wafahamu 'viongozi watatu' wa