Mwanamke afariki kwa kumezwa na injini ya ndege baada ya kukaidi amri kutoisogelea

Mama huyo wa watoto watatu alikuwa mfanyikazi katika uwanja huo wa ndege.

Muhtasari

• Rubani alisema ndege hiyo ilitetemeka sana wakati Edwards alipoingizwa kwenye injini ya kwanza, ambayo ilikuwa bado ikifanya kazi katika kipindi cha dakika mbili kabla ya kupoa.

Courtney Edwards, mwathiriwa aliyefyonzwa na injini ya ndege.
Courtney Edwards, mwathiriwa aliyefyonzwa na injini ya ndege.
Image: NYT

Familia moja ya mama wa watoto watatu nchini Marekani inaomboleza kifo cha uchungu cha mama huyo baada ya kufyonza kwa nguvu na injini ya ndege.

Kulingana na jarida la New York Times, mwanamke huyo alikuwa ni mfanyakazi katika uwanja wa ndege wa Alabama, na kwa muda mrefu alikuwa amepewa tahadhari ya kutokaribia ndege hiyo yenye injini ya nguvu mno.

Mama wa watoto watatu Courtney Edwards, 34, alitambuliwa kama wakala wa kushughulikia ardhi ambaye aliuawa kwenye ajali kwenye Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Montgomery usiku wa kuamkia mwaka mpya.

Alikuwa akifanya kazi kama wakala wa kushughulikia ndege wa Piedmont Airlines, kampuni tanzu ya American Airlines, kulingana na ripoti ya awali kutoka kwa Bodi ya Kitaifa ya Usalama wa Usafiri iliyotolewa Jumatatu.

Ripoti hiyo ilifichua kuwa kabla ya kifo chake, mfanyakazi mwenza alimuona Edwards karibu kuangushwa na moshi wa ndege na kujaribu kumwonya asiende karibu hadi injini zinapozimwa.

Rubani alisema ndege hiyo ilitetemeka sana wakati Edwards alipoingizwa kwenye injini ya kwanza, ambayo ilikuwa bado ikifanya kazi katika kipindi cha dakika mbili kabla ya kupoa.

Wakati wote wa tukio hilo, miale inayozunguka kwenye ndege hiyo ilionekana kuangaziwa, ikionya kwamba injini bado zinaendelea kufanya kazi, wachunguzi walisema.

Ufuatiliaji wa video ulionyesha Edwards akitembea kando ya bawa la kushoto la ndege na mbele ya injini ya kwanza.

“Mfanyakazi mwenza alipiga kelele na kumpungia mkono Edwards. Alianza kuondoka kwenye ndege, lakini akasikia "mlio," na injini ikazima, kulingana na ripoti ya awali,” jarida hilo lilisimulia.