Madaktari wafanikiwa kutoa mpira wa gofu uliokwama kwenye utumbo wa mtoto wa miaka 14

Kijana huyo alikuwa anacheza na mpira huo kabla ya kuuingiza kwenye shmo la makalio yake na ukakataa kutoka.

Muhtasari

• Kijana huyo alijaribu kwenda haja kubwa ili kuutoa mpira huo lakini majaribio yake mara kadhaa yaligonga mwamba.

Mpira wa gofu
Mpira wa gofu
Image: BBC SPORT

Hatimaye madaktari wa upasuaji nchini Australia wameripotiwa kufanikiwa kutoa mpira wa gofu uliokwama kwenye utumbo wa mtoto mmoja wa miaka 14.

Siku kadhaa zilizopita, taarifa za mtoto huyo kudaiwa kuingiza mpira wa gofu kwenye puru (shimo la makalio) yake, ziligonga vichwa vya habari kote duniani, walimwengu wakijumuika kumtilia dua ili mchakato wa kuondolewa mpira huo ukamilike vyema.

Kulingana na ripoti ya jarida la Case Reports in Surgery medical, mvulana huyo aliweka mpira kwenye njia ya haja kubwa na kumfahamisha mama yake alipogundua kuwa hakuweza kuutoa baada ya jaribio lake la kunya kushindikana. Waliwasilisha kwa idara ya dharura ya Hospitali ya Royal Adelaide.

"Hakuwa na maumivu yoyote na aliweza kupita hewa chafu. Mgonjwa alikuwa amejaribu kujisaidia haja kubwa ili kuutoa mpira wa gofu bila mafanikio,” madaktari walisema katika ripoti iliyochapishwa Januari 6.

Baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina kwa kutumia vifaa vya kisasa, mpira huo wa gofu ulionekana ndani kabisa ya utumbo wake mkubwa, mbali na sehemu ambayo ingeweza kufikiwa kupitia upasuaji wa kawaida.

Jaribio la kuutoa mpira huo lilifeli hata baada ya mchakato was aa mbili mfululizo kwa kutumia vifaa tofauti vya udaktari.

Baada ya mbinu zote kufeli, ilichukua ukakamavu wa madaktari kutumia mfumo wa glycoprep ulioasisiwa Ujerumani na ambao ulifanywa kwa njia ya mdomo wa kijana huyo na kusababisha mpira huo kusukumwa nje kupitia haja kubwa, zaidi ya saa 3 baadaye, taarifa ilieleza.

Walibaini kuwa mgonjwa huyo "alibaki akiwa mzima" baada ya kupitisha mpira wa gofu, na alitolewa siku hiyo hiyo.

"Hakukuwa na ushahidi wa jeraha la utumbo. Alishauriwa dhidi ya kuingiza vitu zaidi kwenye puru yake katika siku zijazo,” ripoti hiyo iliongeza.