Dereva wa Waziri Mkuu agonga sanduku la mwanafunzi, amtupia Ksh 300 kama fidia

Dereva huyo baada ya kugonga boksi la mwanafunzi, alimtupia chini Ksh 300 kabla ya kuendesha gari mbio akiondoka eneo la tukio.

Muhtasari

• Ofisi ya Waziri mkuu ililaani kitendo hicho na kusema haiungi mkono hata kidogo huku wakiahidi kuchukua hatua dhidi ya dereva huyo.

Dereva wa waziri mkuu agonga sanduku la mwaanfunzi na kutoroka,
Dereva wa waziri mkuu agonga sanduku la mwaanfunzi na kutoroka,
Image: Maktaba

Dereva wa waziri mkuu wa taifa la Uganda anamlikwa baada ya kudaiwa kugonga sanfuku la mwanafunzi wa shule na kumrushia pesa kidogo kama fidia.

Mwanafunzi huyo alikuwa anarudi shule na dereva huyo aliyetambulika kwa jina Steven Aipikor kulingana na jarida la Monitor nchini humo aligonga sanduku hilo na kumrushia chini shilingi elfu 10 za Uganda sawa za mia tatu za Kenya kabla ya kuendesha gari mbio akienda.

Mwananchi husika alichukua picha ya gari hilo na kuiweka kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Kufuatia fujo kwenye mitandao ya kijamii za Waganda waliokuwa na wasiwasi, waliokuwa wakililia haki kwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Buddo, katibu mkuu katika Ofisi ya waziri mkuu, Bw Keith Muhakanizi, jana alilaani kisa hicho, Monitor walisema.

Bw Muhakanizi katika barua yake alisema ofisi ya waziri mkuu haikubaliani na utovu wa nidhamu na kwamba tayari wameelekeza dereva kuwajibika kwa matendo yake.

“Kama unavyofahamu, Februari 5, 2023, ukiwa unaendesha gari namba UG0915Z mali ya Waziri wa Jimbo la Bunyoro, uliharibu sanduku la mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Budo. Kosa ulilotenda ni kubwa sana na linaichafua sura ya Ofisi ya Waziri Mkuu,” Bw Muhakanizi alimwandikia Bw Aipikor.

Bw Muhakanizi zaidi alihakikishia umma kwamba mipango inafanywa ili kufidia mwanafunzi aliyeathiriwa.