Tajiri apelekwa mahakamani kwa kumsafirisha maskini kwenda Ulaya ili kumuibia figo

Tajiri huyo mwanasiasa alimdanganya maskini huyo mchuuzi wa reja reja kuwa anafadhili ziara yake UK kumbe njama ilikuwa kwenda kuiba figo yake.

Muhtasari

• Binti wa tajiri huyo ndiye alikuwa na figo yake iliyofeli na hivyo alitaka kubandikiziwa figo mbadala.

• Mwaansiasa huyo alimwambia kijana kuwa angempa shilingi milioni moja kwa ajili ya kufanikisha hilo, kijana akakataa na kupiga ripoti polisi

Mwanaume aliyekamatwa
Mwanaume aliyekamatwa
Image: Sagwe

Aliyekuwa naibu rais wa seneti ya Nigeria, mkewe na bintiye walifikishwa katika mahakama ya London siku ya Jumatatu kwa madai ya kupanga kuvuna figo ya mfanyabiashara wa mitaani.

Mwanasiasa huyo kwa jina Ike na Beatrice Ekweremadu, binti yao Sonia mwenye umri wa miaka 25 na daktari, Obinna Obeta, wanatuhumiwa kula njama ya kumnyonya mwanaume huyo kwa ajili ya kiungo chake.

Figo hiyo inadaiwa ilikusudiwa kwa Sonia, ambaye anaendelea kufanyiwa dayalisisi akiwa na tatizo la figo, kwa malipo ya hadi £7,000 ($8,430), sawia na shilingi milioni moja za Kenya na ahadi ya maisha mapya nchini Uingereza kwa mfanyabiashara huyo mwenye umri wa miaka 21.

Kulingana na jarida la AFP, Nchini Uingereza, ni halali kutoa figo, lakini si kwa malipo. Waendesha mashtaka wanasema bila kujali kama mfanyabiashara huyo wa mtaani wa Lagos alitoa kibali chake, uhalifu ulifanywa na matajiri hao wa Nigeria.

Mshtaki huyo -- ambaye jina lake halijatajwa -- anasemekana kwenda kwa polisi wa Uingereza baada ya kukataa kukubaliana na utaratibu huo, kufuatia vipimo vya awali katika hospitali ya kaskazini mwa London mnamo Februari 2022.

Daktari mshauri alisema kijana huyo alikuwa na "uelewa mdogo" wa kwa nini alikuwa huko na "alifarijika" kwa kuambiwa kuwa upandikizaji hautaendelea, mwendesha mashtaka Hugh Davies alisema kulingana na jarida hilo.

Alikuwa amefunzwa kutoa majibu ya uwongo kwa madaktari katika hospitali hiyo, na Sonia alikuwa "akiimba kutoka kwa karatasi ile ile ya nyimbo" ili kuunda historia ya uwongo ya familia inayowaunganisha wawili hao kama binamu, wakili aliambia mahakama.

Ekweremadus na daktari wanatuhumiwa kwa njama kupanga kusafiri kwa mtu mwingine kwa nia ya unyonyaji, chini ya sheria ya Uingereza juu ya utumwa wa kisasa.