Polisi wachunguza kifo cha shabiki wa Man Utd baada ya kufungwa na Liverpool

Kwa bahati mbaya, alifahamishwa baadaye kuwa mwanaye amefariki . Alipatikana akiwa amefariki kitandani kwake.

Muhtasari
  • Mwanaume huyo Eddy Okello, ambaye ni dereva na mkaazi wa eneo la Okwor Okwor Cell, mjini Lira, alipatikana akiwa amefariki
Crime Scene
Image: HISANI

Shabiki wa Manchester United katika mj wa Lira , kaskazini mwa Uganda , alifariki katika mazingira ya kutatanisha baada ya kutazama mechi ya soka Jumapili ambapo timu anayoienzi iliaibishwa kwa kuchapwa na Liverpool 7-0 katika mchezo wa Ligi ya Primia ya Uingereza, limeripoti gazeti la Daily Monitor nchini humo.

Mwanaume huyo Eddy Okello, ambaye ni dereva na mkaazi wa eneo la Okwor Okwor Cell, mjini Lira, alipatikana akiwa amefariki katika chumba chake Jumatatu mchana .

Msemaji wa polisi kanda ya North Kyoga, SP Patrick Jimmy Okema, amethibitisha tukio hilo, akisema kuwa uchunguzi unaendelea kubaini sababu halisi ya kifo.

"Uchunguzi wa awali wa polisi unaonyesha kuwa Okello aliondoka nyumbani kwake saa kumi na mbili na nusu jioni , tarehe 5 Machi kutazama mechi katika kituo Jirani cha kibiashara.

Alirejea nyumbani saa tatu unusu usiku. Mama yake alimpatia chakula cha usiku, lakini hakuweza kula , akisema kuwa hakuwa anahisi vizuri.

Kwahiyo, aliingia ndani na kulala ," Bw Okema alinukuliwa na gazeti la daily Monitor akisema Jumatatu jioni.

Aliongeza kuwa Jumatatu majira ya saa tatu unusu asubuhi, baba yake marehemu alisikia simu yake ikilia kutoka ndani ya nyumba ya Okello, akashangaa ni kwanini hakwenda kufanya kazi, lakini aliamua kutomsumbuaakidhani kuwa huenda alikuwa bado anapumzika.

Kwa bahati mbaya, alifahamishwa baadaye kuwa mwanaye amefariki . Alipatikana akiwa amefariki kitandani kwake.