Kingi aidhinisha mabadiliko ya uongozi wa wachache katika seneti

Ole Kina alichukua nafsi ya seneta wa Isiolo, Fatuma Dullo

Muhtasari

•Kingi alikaa kwa muda  ili kuidhinisha nafasi hizo tangu Odinga kutangaza mabadiliko hayo.

LEDAMA 2
LEDAMA 2

Spika wa Seneti, Amason Kingi, ameidhinisha mabadiliko katika uongozi wa wachache katika Seneti.

Kingi  siku ya Alhamisi alitangaza kuwa Seneta wa Narok Ledama Ole ndiye kiranja wa wachache bungeni na  seneta wa Nairobi, Edwin Sifuna naibu wake.

Kingi aliongezea kuwa Fatuma Dullo alikuwa katika safari inayohusiana na shughuli za bunge na hivyo aliwataka viongozi hao wapya kutokuwa na pupa ya kuingia afisini akidai kuwa vitu vya Fatuma bado vilikuwepo afisini humo na kuwaeleza wawe na subira hadi pale atakapofika.

Kiongozi wa muungano wa Azimio, Raila Odinga awali alikuwa ametangaza mabadiliko ya uongozi wa wachache katika Seneti na kumteua seneta wa Narok, Ledama Ole Kina kuwa kiranja mpya wa wachache.

Odinga alitangaza mabadiliko hayo tarehe 15 Februari katika mkutano na maseneta wa Azimio.

Ole Kina amechukua nafasi  ya seneta wa Isiolo Fatuma Dullo.Edwin Sifuna  atakuwa naibu wa seneta wa Narok,Ledama Ole Kina.

Odinga pia alithibitisha kuwa Seneta wa Kilifi Steward Madzayo atasalia Kiongozi wa Wachache katika Seneti, huku Seneta wa Kitui Enock Wambua akiwa naibu wake.

Waziri Mkuu huyo wa zamani alisema kuwa mabadiliko hayo yalilenga kuimarisha utendakazi na ajenda ya muungano wa Azimio katika bunge la juu, pamoja na kustawisha umoja na ushirikiano miongoni mwa maseneta.

“Tumewaomba wajumbe wetu kuendelea kuiwakilisha Azimio ipasavyo katika Bunge. Azimio anasimamia utetezi wa watu wa Kenya,” Odinga alisema.