Wakimkamata Raila wameshika nchi nzima-Karua awaonya polisi

Awali Msafara wa Raila Odinga warushiwa vitoa machozi Kawangware Nairobi

Muhtasari
  • Aliwataka zaidi wafuasi wa Azimio kutolegea huku wakishinikiza utawala wa Rais William Ruto kutii matakwa yao.
RAILA ODINGA NA MARTHA KARUA
Image: ANDREW KASUKU

Kiongozi wa Narc Kenya Martha Karua alionya dhidi ya mipango ya kumkamata kiongozi wa ODM Raila Odinga.

Akihutubia wananchi wakati wa maandamano ya Azimio Jumatatu, Karua alisema jaribio lolote la kumkamata Raila litakuwa balaa kwa nchi.

Karua alidai kuwa kuna njama za kutaka kiongozi huyo wa ODM azuiliwe na polisi.

"Mimi nataka muelewe wakona mpango ya kushika Baba. Wakimguza watakuwa wameguza Kenya,"Karua alizungumza.

Aliwataka zaidi wafuasi wa Azimio kutolegea huku wakishinikiza utawala wa Rais William Ruto kutii matakwa yao.

""Kwa hivyo tuendelee adi tutoboe hii safari ."

Siku ya Jumapili, Inspekta Jenerali wa Polisi Japhet Koome alionya dhidi ya hatua zozote za watu wengi na mikusanyiko ya maandamano akisema ni kinyume cha sheria.

Koome alisema polisi watawatendea kila mtu kwa usawa wakati wa kuwakamata waandamanaji mitaani.

Awali Msafara wa Raila Odinga warushiwa vitoa machozi Kawangware Nairobi

Msafara wa kiongozi wa Muungano wa Azimio Azimio La Umoja One Kenya Raila Odinga siku ya Jumatatu ulijitokeza kupitia eneo la Kawangware jijini Nairobi ili kuendeleza maandamano ya pili dhidi ya serikali.

Odinga aliambatana na naibu wake katika Muungano wa huo Martha Karua, kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka na kiongozi wa chama cha Roots Party George Wajackoyah, miongoni mwa viongozi wengine wa upinzani.