Rais mteuleTinubu kuapishwa licha ya kesi mahakamani

Wagombea wanne wa urais waliwasilisha mapingamizi ya kisheria tarehe 21 Machi dhidi ya ushindi wa Bw Tinubu,

Muhtasari
  • Bw Mohammed alisema "hakuna msingi" wa katiba ya serikali ya mpito.Alisema vyama vya siasa vya upinzani vina haki ya kupinga uchaguzi wa urais mahakamani

Waziri wa Habari wa Nigeria Lai Mohammed anasema rais mteule Bola Tinubu ataapishwa tarehe 29 Mei licha ya kesi mahakamani kupinga ushindi wake.

Makundi ambayo hayajaridhishwa na matokeo ya uchaguzi wa urais wa tarehe 25 Februari yanaitisha serikali ya mpito huku Rais anayemaliza muda wake Muhammadu Buhari akiondoka madarakani rasmi mwezi Mei.

Bw Mohammed alisema "hakuna msingi" wa katiba ya serikali ya mpito.Alisema vyama vya siasa vya upinzani vina haki ya kupinga uchaguzi wa urais mahakamani

Wagombea wanne wa urais waliwasilisha mapingamizi ya kisheria tarehe 21 Machi dhidi ya ushindi wa Bw Tinubu, kwa madai kuwa kulikuwa na wizi wa kura na udanganyifu .

Inachukua takriban miezi minane kwa mahakama kuamua ombi la uchaguzi wa urais.Ombi lazima lisikilizwe ndani ya siku 180 tangu siku lilipowasilishwa.

Mlalamishi anaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama katika Mahakama ya Rufaa ndani ya siku 21 kutoka tarehe ya uamuzi.

Iwapo walalamikaji hawajaridhika na uamuzi wa mahakama ya rufaa, unaotolewa ndani ya siku 60, wana siku 21 za kukata rufaa katika Mahakama ya Juu, ambayo uamuzi wake ni wa mwisho.