Mashindano ya watoto ya kuua paka New Zealand yaahirishwa

Tukio hilo lilileta shutuma kutoka kwa vikundi vya ustawi wa wanyama.

Muhtasari

•Waandaaji wa msako wa kila mwaka walikosolewa baada ya kutangaza kitengo kipya cha watoto kuwinda paka mwitu nchini New Zealand.

Image: bbc

Mashindano ya watoto ya kuwinda paka nchini New Zealand yamehirishwa kufuatia mvutano kuhusu tukio hilo. Waandaaji wa msako wa kila mwaka walikosolewa baada ya kutangaza kitengo kipya cha watoto kuwinda paka mwitu nchini New Zealand.

Vijana waliambiwa wasiue wanyama wa kufugwa, lakini walihimizwa vinginevyo waue paka wengi wa mwituni ili wapate zawadi ya NZ$250 (£124; $155). Tukio hilo lilileta shutuma kutoka kwa vikundi vya ustawi wa wanyama.

Siku ya Jumanne, Jumuiya ya Kuzuia Ukatili kwa Wanyama ya New Zealand ilisema kuwa imefarijiwa "mpango wa watoto ambao ulihusisha kuwapiga risasi paka mwitu" hautaendelea.

Mwakilishi alisema kuwa watoto, pamoja na watu wazima, hawataweza kutofautisha kati ya "paka mwitu, mpotevu au anayefugwa", kulingana na AFP. Pia kumekuwa na hofu kwamba paka wa nyumbani wanaweza "kunaswa kwenye mashambulii", mfadhili wa zamani wa uwindaji huo alikiambia chombo cha habari cha Stuff.