logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jina la 'Pele' laingizwa rasmi kwenye Kamusi

Kamusi ya Michaelis ya lugha ya Kireno, ni moja ya kamusi maarufu zaidi nchini Brazili

image

Habari27 April 2023 - 11:25

Muhtasari


  • Kuingizwa kwa jina lake kwenye kamusi kulikuja baada ya kampeni ya Pelé Foundation ya kumuenzi nyota huyo wa kandanda kukusanya saini zaidi ya 125,000.

Pelé, ambalo ni jina la utani la gwiji wa soka marehemu Edson Arantes do Nascimento, limeingizwa rasmi kwenye kamusi likimaanisha kitu ama jambo la "kipekee, kisicholinganishwa".

Kamusi ya Michaelis ya lugha ya Kireno, ni moja ya kamusi maarufu zaidi nchini Brazili, iliongeza "pele" kama kivumishi kipya.

Kuingizwa kwa jina lake kwenye kamusi kulikuja baada ya kampeni ya Pelé Foundation ya kumuenzi nyota huyo wa kandanda kukusanya saini zaidi ya 125,000.

Pele alifariki mnamo Disemba akiwa na umri wa miaka 82. Gwiji huyo pekee aliyeshinda Kombe la Dunia mara tatu, anachukuliwa kuwa mwanasoka bora zaidi kuwahi kutokea duniani, katika historia.

Wakati wa uchezaji wake wa miongo miwili, alifunga mabao 1,281 akiwa na klabu ya Santos ya Brazil, timu ya taifa ya Brazil na New York Cosmos.

 

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved